HIVI NDIVYO UNAWEZA IFAHAMU NYOTA YAKO KAMA IMEIBIWA AU KUCHAFULIWA

Katika mada yetu ya leo tutaangazia baadhi ya mambo yanayoweza kuashiria kama nyota yako imeibiwa au kuchafuliwa.  Vipo vitu vingi vinavyochangia kuibiwa nyota yako na kupelekea kuharibiwa, kuchafuliwa na kufa kabisa. 

Hivyo basi katika kulitambua hilo, tukaona ni vyema tuviorodheshe ili uweze kufahamu na kujtathimini upo katika kundi lipi kati ya haya.

  •  UZINZI : Vitabu vyote vya mafundisho ya imani zote mbili, hapa nazungumzia Uislamu na Ukristo vinatoa onyo kali juu ya mtu mzinzi.  Hii inatupa picha ya kwamba kitendo hiki ni batili na huchangia kuleta uharibifu kwetu sisi wanadamu kama vile maradhi, kuharibu na kuchafua nyota endapo ikatokea mtu uliyezini nae akawa na nuksi mwilini mwake.
  • KUROGWA NA WACHAWI : Silaha kubwa ya adui ili aweze kukushinda ni kufahamu mapungufu au madhaifu yako.  Wanachokifanya wachawi kabla ya kukuroga ni kutazama uimara wa nyota yako na endapo wakapata upenyo wa kuona walau madhaifu madogo basi hutumia mwanya huo kuweza kuharibu nyota yako kisha kukuroga na kukuchezea kadri wawezavyo.
  • KUHARIBIKA KWA MIPANGO YAKO : Kama kuna mipango au mikakati madhubuti uliyojiwekea basi ndugu yangu utashangaa mmoja baada ya mwingine unakufa na kupotea kabisa, hata kama ilitokea uliahidiwa kupata kazi au kupandishwa cheo matarajio hayo huyeyuka na kupotea kama upepo.
  • BIASHARA KUYUMBA : Ikiwa ulikuwa na biashara yako inafanya vizuri kwa kupata wateja na kukuingizia faida, utaanza kuona mabadiliko taratibu ya mtaji kuyumba na duka kufa bila kufahamu hela umepeleka wapi, hata kama kuna watu uliwakopesha mahitaji unaweza kushangaa ukawasahau kabisa hata majina yao.
  • MAHUSIANO KUVUNJIKA : Yaani hapa kila kitu kinakuwa shaghala baghala, unaweza ukamkufuru hata Muumba wako. Kama ulikuwa katika uchumba au ndoa utashtukia imevunjika pasipokuwa zile sababu za msingi zinazopelekea kuvunjika kwa mahusiano mengi kama vile usaliti, wivu au ugomvi.

Leave a comment