JINSI YA KUMVUTA NA KUMRUDISHA MPENZI WAKO HARAKA

Huu ni Utaalamu mwepesi wa jinsi ya Kumvuta Mpenzi wako ambaye aidha hakupendi au amekutoroka.

Mapenzi Haraka

Utaalamu huu utakupa uwezo wa kuvuta Mapenzi ya aina yoyote kwa Mpenzi wako, Marafiki zako, Wafanyakazi wenzio, Wakubwa wako wa kazi, Ndugu zako Adui zako na kwa ujumla mtu yoyote ambaye unataka akupende.
Vitu vinavyohitajika ni kama ifuatavyo:

1. Karatasi Nyeupe kabisa isiyo na Mistari na ambayo haijatumiwa (Karatsi Mpya)
2.Kalamu mbili za Wino, moja Nyeusi na moja Nyekundu.
3.Maua ya Waridi (Rose Flower) mawili ya rangi ya Pinki.
4.Jagi la Maji la Kioo likiwa na maji karibu kujaa.
5.Mkasi mpya Mdogo ambao haujatumika.
6.Bakuli la Maji likiwa na maji ndani yake.

KAZI HII UNAIFANYA WAKATI GANI?

Shughuli hii unatakiwa uifanye wakati wowote ambao wewe mwenyewe unahisi kwamba haupendwi. Haina wakati maalum
JINSI YA KUFANYA :

Kata karatasi hiyo Nyeupe katika vipande viwili vilivyo sawa, hakikisha umepima, ili kimoja kisizidi kingine.

KWA KUMVUTA MPENZI:

•Ukitumia Kalamu Nyekundu, andika katika moja ya vipande hivyo viwili vya karatasi kwa ufupi mambo yote ambayo unafikiri yanakufanya upendwe na watu, mfano, labda una sura nzuri, au unavaa vizuri, au unasaidia sana watu au unazungumza na Watu vizuri na Kadhalika.

•Chukua karatasi uliyoandika maneno yako mazuri, iweke dirishani Maandishi yaelekee Juu, Juu yake weka Jagi la maji la Kioo. Ndani ya Jagi tia yale maua mawili ya Waridi (Rose), Wakati unaweka Maua hayo unatakiwa unuie na uwataje kwa majina yao wale unaowataka wakupende au jambo unalolitaka la Mapenzi.

•Karatasi ya mambo yako mazuri uliyoiweka chini ya Jagi la maji iache hapo mpaka Mwezi utakapoandama, unachotakiwa kufanya, nikubadilisha mara kwa mara Maua yaliyo ndani ya Jagi kila unapoona yamenyauka.

KWA KUJISAFISHA NA KUJITOA MIKOSI

•Ukitumia Kalamu Nyeusi, andika katika kipande cha karatasi kilichobaki mambo yote Ambayo unafikiri yanawafanya watu wakuchukie, Mfano: Kama pengine wewe ni Jeuri, au una sura mbaya, au labda wewe ni mbahili au labda unaringa sana na kadhalika.

•Karatasi uliyoandika mambo yako mabaya itie ndani ya bakuli la maji na uiache hapo mpaka maandishi uliyoandika kwa Wino mweusi yafutike kabisa, kisha ulitupe karatasi lililolowa ambalo litakuwa halina maandishi Kwenye Jalala la Taka.
Maji ya kwenye Bakuli yamwage njia panda, wakati wa kiza (Usiku). Unapomwaga Utie nia kwamba usichukiwe tena na haowanaokuchukia.

Fanya hivyo na utaona Maajabu.

Wale watakaofanya utaalamu huu tunawaomba watume Mafanikio gani waliyopata na kitu gani kilichotokea baada ya kufanya tendo hilo kupitia : +255 789 41 95 57

Wabillah Tawfiq

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s