BINTI WA KIISLAMU ALIYEVULIWA HIJAB NA POLISI ALIPWA MAMILIONI YA FEDHA

Kristy Powell

Mwanamke mmoja Muislamu ambaye alilazimishwa kuvua hijab yake na maafisa wa polisi mjini California amezawadiwa $85,000 (£65,000).

Kirsty Powell aliwasilisha kesi mahakamani dhidi ya baraza mji wa Long Beach baada ya kulazimishwa kuvua vazi lake la hijab kufuatia kukamatwa kwake 2015.

Ombi la Bi Powell la kutaka kuhudumiwa na afisa wa polisi mwanamke lilipuuzwa na akalazimika kulala jela bila hijab yake.

Idara hiyo sasa imebadili sera yake kuhusu mavazi ya kidini ya kichwani.

Maafisa wa kike sasa wanaruhusiwa kuondoa hijab zao mbali na maafisa wa kiume na wafungwa iwapo usalama wa maafisa hao unatishiwa, alisema jaji wa Long Beach Monte Machit akizungumza na gazeti la Los Angeles Times.

Hata hivyo baraza la mji wa Long Beach lilikubali kumaliza kesi hiyo kulingana na baraza la mahusiano ya waislamu .

Baraza hilo ambalo lilianzisha kesi hiyo lilisema kuwa maafisa wa polisi kwa lazima walivua hijab yake mwanamke huyo mbele ya maafisa wa polisi wanaume na makumi ya wafungwa.

-CREDITS : BBC Swahili

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s