FAHAMU MAMBO MAKUU 5 AMBAYO UKIOLEWA LAZIMA UACHANE NAYO

Ndoa

(1) KUENDELEA KUWASILIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI; 

Huyu hana nia nzuri na wewe, mlishaachana hata kama ni ile kuachana kwa wema lakini kuna mawili, ukimchekea sana atazini na wewe, lakini mumeo akijua anakutimua.

Nikiamini kuwa labda kama mumeo hakupendi ndiyo atakucha ujichekeshe chekeshe na mpenzi wako wa zamani, ila kama anakupenda kakutimua, hawezi vumilia, hivyo achana naye usimfuatilie wala usiwasiliane naye, and yes msiwe marafiki. Vile viofa ofa anavyokupa hembu achana navyo kwani siku ukiachika basi nayeye humuoni tena.

(2) KUMUELEZEA MAMA YAKO KILA KITU KINACHOKUTOKEA; 
Mwanzoni ulikua unamuelezea siri zako, sasa hivi una mume, kila unachomuambia kinawahusu nyie wawili, kwanza unamvua nguo mumeo na pili akijua kua kila kitu ni kwa Mama, kila maamuzi ni mpaka Mama akubali atajiona kama hajakuoa wewe kamuoa Mama yako.

(3) KUELEZA SIRI ZA FARAGHA KWA RAFIKI ZAKO:
Hawa watakuibia na sisi wanaume kwakua hatujivungi, ukikaribishwa chakula cha bure unakula tu, hivyo acha kabisa ushakua mtu mzima kufikishwa kileleni ndiyo nini! Unafikiri wao hawataki?

Mnaharibu ndoa zenu kwakua hamuishi kuwasifia hao waume zenu, tena wengine hata kwa sifa za uongo. Sasa wanaume wazuri wanaojali ni washida hivyo shoga yako akisikia unaye atasema hata mimi nilikua namtafuta huyo huyo na atamchukua bila hata kupepesa macho.

(4) ACHA KWENDA KULIA SHIDA KWENU:  
Kila shida unayopata kwenu, kumuambia Mama, yaani mume hata hajasema siwezi, hajakutuma au ni kitu cha kununua kakuambia hana hela umeshaenda kulia lia kwenu kwakua wana uwezo. Hapo utamfanya mumeo asijihisi kama mwanaume na atatafuta tu mwanamke wa kumfanya ajihisi mwanaume.

Acha huo ujinga, muache mume wako ajaribu kutatua mpaka ikishindikana na yeye akakuambia mke wangu hapa hili ni kubwa sana tukaombe msaada. Lakini kama kila kitu kidogo ni kwenda kwenu atakuchoka na kukukimbia kwani ataona kama yeye hana maamuzi, unamuona kama hawezi kutunza familia mpaka asaidiwe na wakwe.

(5) KUTUMIA MUDA MWINGI SANA NA MARAFIKI ZAKO:

Umeolewa lakini kuna wale rafiki zako ambao bado wana danga unataka uendelee kutoka nao kila siku, kuwakaribisha nyumbani kwakua hawana kazi wanakuja na kukaa tu, asubuhi jioni mume akirudi anawakuta.

Jingine huwaingiza mpaka chumbani, mnavaliana na nguo, yaani mke wa mtu unavaliana nguo na mwanamke mwingine! Wewe moja kwa moja hujajua maana ya ndoa ni nini?

Umeolewa ni lazima ujiheshimu, sisemi uwatenge hapana, mbakie marafiki lakini kuwe na mipaka, wewe waendekeze tu kuna mawili, mume atatembea nao au atachoka tabia zao atawachukia na kukuchukia na wewe.

Unasumbuliwa na Mume/Mpenzi/Mchumba? Anashindwa kutimiza ahadi? Mmeachana na unataka kumrudisha? Wasiliana na Dokta Sule : +255 658 87 20 26

NB: Rafiki zako wanapaswa kuishi sebuleni kwako na kamwe wasikanyage chumbani!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s