UMUHIMU WA KUOMBA DUA

Msaafu

ADABU ZA KUOMBA DUA

1. Usafi wa mwili : Kwa sababu Dua ni Ibada, na Ibada haikubaliki bila ya usafi.

2.Kuinua mikono juu wakati wa kuomba Dua : Amesema Mtume (swalla Allah alayhi wasallam) : “Hakika Mola wenu ana sifa ya haya na ukarimu. Anaona haya kumrejesha mja wake anapoinua mikono yake kumuomba Dua” (Bukhariy).

3. Kuomba Dua zilizothibiti katika Qur’an na Sunna ya Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam).

NYAKATI ZA KUKUBALIWA DUA

A. Wakati wa kusujudu. Amesema Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam): “Mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake wakati akiwa katika sijida. Kwa hivyo, ombeni Dua wa wingi” (Muslim).

B. Baada ya Adhana. Amesema Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam): “Dua hairejeshwi baina ya Adhana na Iqaama” ( At-Tirmidhi).

C. Thuluthi ya mwisho wa usiku. Amesema Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam): “Mola wetu anateremka kila usiku mpaka katika uwingu wa dunia wakati wa thuluthu ya mwisho wa usiku. Na Anasema: Nani mwenye kuniomba nimkubalie dua yake” ( Bukhari).

D. Siku ya Ijumaa: Amesema Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam): “Katika siku ya Ijumaa kuna Saa, atakaye omba Dua. Mwenyezi Mungu hukubali dua yake] (Bukhari na Muslim).

E. Wakati wa kunywa maji ya zamzam : Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam) anasema “Maji ya zamzam kwa (jambo liloombewa) wakati wa kunywa” Sahih Ibn Maajah.

F. Dua wakati wa neema : Amesema Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam): “Mwenye kutaka ajibiwe na Allaah wakati wa shida na dhiki azidishe duaa wakati wa neema” at-Tirmidhiy na al-Haakim.

Tujitahidini katika kumuomba Allah (subhanahu wataala) kwa ikhlaas na kwa kuwa na yaqini dua zetu zitakubaliwa na msitusahau katika dua zenu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s