NASAHA 40 ZITAKAZO IMARISHA NDOA YAKO

ndoa ya kiislamu
1 – Chagua mke/mume mwema .
2- Kama umekosea katika kumchagua mke mwema basi fanya haraka kumfanya awe mwema huyo uliyenaye.
3- Ifanye nyumba yako kuwa ni mahali pa kutajwa mwenyezi mungu(subhaanahuu wataala).
4- Ifanye nyumba yako kuwa ni Qibla(mahali panaposwaliwa).
5- Ilee familia yako kiimani.
6- Kutilia umuhim juu ya adhkaari za kisheria na sunna zinazofungamana na nyumba ikiwa ni pamoja na dua za kuingia na kutoka kwenye nyumba.
7- Kuunganisha kuisoma suratul baqara kwenye nyumba kwaajili ya kufukuza mashetani ndani yake.
8- Kuwafunza na kuwafundisha wanafamilia dini yao.
9- Tengeneza maktaba ndogo ya vitabu vya dini nyumbani kwako.
10- Weka maktaba ya sauti nyumbani kwako(kaseti na sidii mbali mbali za kielimu)
11- Waalike nyumbani kwako watu wema , masheikh na maustadhi mbali mbali kutembelea nyumbani kwako.
12- Ifundishe familia yako hukumu mbali mbali za kisheria.
13- Toa fursa kwa wanafamilia kujadili mambo mbali mbali ya kifamilia.
14- Usionyeshe tofauti za kifamilia mbele ya watoto.
15- Usimuingize nyumbani kwako mtu ambaye huridhishwi na dini yake.
16- Ijue familia yako vizuri , kwa kuwajua marafiki wa watoto wako, mumeo/mkeo , mfanyakazi wa ndani .
17- Tilia umuhimu malezi ya watoto.
18- Panga nyakati maalum kwaajili ya chakula na kulala.
19- Pangilia kazi za mke nje ya nyumba.
20- Hifadhi na linda siri za familia.
21- Hubiri upole kwa wanafamilia na wasifanye mambo kwa kutumia maguvu.
22- Wasaidie watu wa nyumbani kwako katika kazi za nyumbani.
23- Jenga urafiki na kila mwanafamilia na toa fursa za utani wa hapa na pale , utani ulio ndani ya mipaka ya nidhamu na heshima.
24- Piga vita tabia zozote mbaya ndani ya nyumba.
25- Tundika bakora mahali ambapo wanafamilia watakuwa wakiiona.
26- Jihadhari kuwaingiza nyumbani ndugu wa karibu wa familia ambao si maharim hasa hasa mmoja wa nguzo za familia asipokuwepo .
27- Tenganisha kati ya wanaume na wanawake katika ziara za kifamilia.
28- Kuwa mwangalifu na wafanyakazi wa ndani , wakike na wakiume.
29- Kama kuna wanaume wajifananishao na wanawake watoe ndani ya nyumba .
30- Zingatia matumizi mazuri ya Televisheni .
31- Jihadhari na shari za simu .
32- Ondoa kila ambacho ni alama ya dini batili au viabudiwa vyao.
33- Zuia na kataza uvutaji sigara ndani ya nyumba.
34- Jiepushe na ufugaji mbwa katika nyumba.
35- Ondoa na toa ndani ya nyumba mapicha yote ya viumbe vyenye roho, sawa sawa viwe ukutani au kwenye albamu.
36- Angalia mahali pazuri pa kujenga nyumba yako , kama eneo la karibu na mskiti.
37- Kuwa na nyumba nzuri , yenye nafasi ya kutosha na kipando kizuri chenye kuvutia kwani hivi ni miongoni mwa vitu vinavyoleta furaha ya maisha.(dala dala mpaka lini?)
38- Chagua jirani kabla ya kujenga nyumba sehemu uliyopata kiwanja.
39- Tilia umuhimu upatikanaji wa vitu muhimu kwenye nyumba na eneza njia zote zinazoleta raha kwenye familia.
40- Chunga sana juu ya afya za wanafamilia na zingatia misingi ya amani kwenye nyumba.
Hizi ni nasaha 40 ambazo ukizizingatia na kuzifanyiakazi basi nyumba yako itakuwa ni nyumba yenye amani na furaha kwa urefu wa umri wako duniani.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s