MAMBO UNAYOPASWA KUYAFANYA SIKU YA IJUMAA

Makka

Allah Anasema :-

( *يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ )*

الجمعة (9) Al-Jumu’a

((Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.))

*Kukoga (Ghuslu)* :-
Ni Wajibu (sunna iliyotiliwa nguvu)

📖Kwa kuthibiti Dalili :-

حديث أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم
قَالَ: *الْغُسْلُ يَوْمَ الْجُمُعَةِ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُحْتَلِم*ٍ. أخرجه البخاري

_Kutoka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriy ambaye alisema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema Ghuslu (kukoga kwa kujitia twahara) siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila Muislamu aliyebaleghe._
[Al-Bukhaariy]
2⃣Inapendekezwa kwa kila anayekwenda kuswali *kujisafisha,* *kupiga* *mswaki,* *kujitia mafuta mazuri* (isipokuwa mwanamke) na *kuvaa nguo iliyo nzuri kabisa*.

Muislamu akitimiza adabu ya Swalah ya Ijumaa hufutiwa madhambi yake ya wiki.

📖Kwa kuthibiti Dalili :-

عن سلمان رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم
*لا يغتسل رجل يوم الجمعة، ويتطهر ما إستطاع من طهر، ويدّهن من دهنه، أو يمس من طيب بيته، ثم يخرج فلا يفرق بين إثنين، ثم يصلي ما كتب له، ثم ينصت إذا تكلم الإمام، إلا غفر له ما بينه وبين الجمعة الأخرى*
. رواه البخاري

_Kutoka kwa Salmaan رضي الله عنه ambaye alisema: Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم “Muislamu atakayekoga (Ghuslu) siku ya Ijumaa, akajisafisha vizuri awezavyo, akatia rangi (nywele zake) (isiyo nyeusi), au akajipaka mafuta mazuri aliyonayo nyumbani kwake, kisha akaenda Msikitini bila ya kufarikisha (kuwapangua akipita) watu wawili (ambao wameshakaa kitako msikitini), akaswali aliyofaridhishwa, kisha akasikiliza (khutbah) kimya, hufutiwa madhambi yake yaliyo baina ya Ijumaa hiyo na Ijumaa ijayo._

[Al-Bukhaariy na Ahmad]

3⃣ *Swalah Ya Ijumaa*

Allaah سبحانه وتعالى Ametuamrisha kwenda kuswali Swalah ya Ijumaa

َ*يا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِي لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ*

“_Enyi mlioamini! Ikiadhiniwa Swalah siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Allaah, na acheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua_

” [Al-Jumu’ah 62: 9]
Ni wajibu kwa kila *mwanamme Muislamu* kwenda kuswali Ijumaa, na hatari ya kutokwenda kuswali bila ya kuwa na sababu iliyoruhusu shari’ah ni kuwa Allaah سبحانه وتعالى humpiga muhuri mtu moyoni mwake, kama katika Hadiyth sahihi ifuatayo:

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: *من ترك ثلاث جمع تهاونا طبع الله على قلبه*
. رواه أحمد وأصحاب السنن

_Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم : Atakayeacha (kuswali Swalah ya) Ijumaa mara tatu bila ya sababu yeyote, Allaah سبحانه وتعالى humpiga muhuri katika moyo wake_

.” [Ahmad na wapokezi wa Hadiyth wengine wenye vitabu vya ‘Sunnan’]

Kupigwa muhuri huo inamaanisha kwamba Allaah سبحانه وتعالى Ameshampa chapa huyu mtu kuwa ni ‘Aasi na amekwishatumbukia katika makemeo ya Allaah سبحانه وتعالى kwamba ni katika walioghafilika kama alivyotutahadharisha Mtume صلى الله عليه وسلم:

حديث ابن عمر وأبي هريرة رضي الله عنهما المخرج في صحيح مسلم من أنهما سمعا رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول على أعواد منبره: *لينتهين أقوام عن ودعهم الجمعات أو ليختمن الله على قلوبهم ثم ليكونن من الغافلين*

Kutoka kwa Ibn ‘Umar na Abu Hurayrah رضي الله عنهما kwamba wamemsikia Mtume صلى الله عليه وسلم akisema:
_“Wasiohudhuria Swalah ya Ijumaa wabadilishe mtindo wao huo au sivyo Allaah سبحانه وتعالى Atawapiga mihuri katika nyoyo zao na watakuwa miongoni wa walioghafilika_
.” [Muslim]

4⃣ *Kufika Mapema Msikitini*

Kila atakapofika mtu mapema msikitini huwa amepata daraja Fulani na muhimu kabisa ni kufika kabla ya khutba kuanza, akichelewa mtu kufika akakosa khutba atakuwa amekosa Swala ya Ijumaa.

حديث أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم
قَالَ: *مَنِ اغْتَسَلَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ غُسْلَ الْجَنَابَةِ ثُمَّ رَاحَ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَدَنَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّانِيَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَقَرَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّالِثَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ كَبْشًا أَقْرَنَ، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الرَّابِعَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ دَجَاجَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الْخَامِسَةِ فَكَأَنَّما قَرَّبَ بَيْضَةً، فَإِذَا خَرَجَ الإِمَامُ حَضَرَتِ الْمَلاَئِكَةُ يَسْتَمِعُونَ الذِّكْرَ.*
أخرجه البخاري

Kutoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه ambaye alisema: Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: “
_Atakayekoga (Ghuslu) siku ya Ijumaa kisha akaenda Msikitini, itakuwa kama mfano ametoa (kafara ya) *ngamia.* Akienda saa ya pili yake, itakuwa kama katoa (kafara ya) *nġ’ombe.* Akienda saa ya tatu yake, itakuwa kama katoa (kafara ya) *kondoo mwenye pembe* Akienda saa ya nne yake, itakuwa kama katoa *kuku*. Akienda saa ya tano yake itakuwa kama *katoa yai*. Imaam akifika, Malaika watatoka kuja kusikiliza dhikr_
[Al-Bukhaariy]

6⃣ *Kusoma Suratul-Kahf*

Wanachuoni wengi wanaonelea kuisoma Suratul-Kahf siku ya Ijumaa kutokana na Hadiyth ifuatayo chini,

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم 
قال: *من قرأ سورة الكهف يوم الجمعة أضاء له من النور ما بين الجمعتين*
. رواه الترمذي

Kutoka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriy رضي الله عنه ambae alisema: Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم : _Atakayesoma Suratul-Kahf siku ya Ijumaa atakuwa katika mwangaza baina ya Ijumaa mbili_
.” [At-Tirmidhiy]

· 7⃣ *Kumswalia Mtume صلى الله عليه وسلم*

عن أوس بن أوس رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم 
*إن من أفضل أيامكم يوم الجمعة، فأكثروا علي من الصلاة فيه، فإن صلاتكم معروضة علي*
. رواه أبو داود

Kutoka kwa Aws Ibn Aws رضي الله عنه ambaye alisema: Kasema Mtume صلى الله عليه وسلم: “
Siku bora kabisa kwenu ni siku ya Ijumaa, kwa hiyo zidisheni kuniswalia, kwani Swalah (kuniombea) zenu zinaonyeshwa (zinaletwa mbele yangu) kwangu._
” [Abuu Daawuud]

*واللهُ أعلمُ*

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s