KISA CHA NABII SULEIMAN

Nabii suleiman

Wakati mmoja enzi za nabii suleiman a.s alijiwa na mmoja wa ndege akamwambia, “Ewe nabii wa m/mungu hakika mm nimetoka sehm moja ktk jangwa fulani nikaona athari ya mji wa ajabu”.

Nusu umefunikwa na mchanga na unaonekana kidogo sehm moja iliyobaki,mji huo ni mji wa ajabu. Nyumba zake zimejengwa kwa dhahabu na madini mengine.

Nabii suleiman a.s akamwambia yule ndege ampeleke ktk huo mji uliozikwa. Akakusanya Akayakusanya majeshi yake binadamu,majini na upepo. Wakaenda mpk wakafika ktk mji huo uliokuwa umefukiwa na mchanga.

Nabii suleiman a.s akaona athari ya mji ukiwa nusu lkn umefukiwa na mchanga. Akauamrisha upepo uufukue ule mji,,,ulipofukuliwa mji ule nabii suleiman akashangaa kuona majumba yaliyojengwa kwa dhahabu.

Akaingia ndani ya mji ule,,,alipoingia tu akalikuta moja la fuvu la binadamu. Nabii suleiman a.s akalishika lile fuvu akalipiga kidogo kichwani akiliamrisha liongee kwa uwezo wa m/mungu.

Likaongea lile fuvu kwa uwezo wa m/mungu,,nabii suleiman akaliuliza lile fuvu kuwa wao ni wakina nani. Lile fuvu likasema kuwa wao ni wamoja kati ya watu waliopita nyuma,,,m/mungu aliwapelekea mtume lkn hawakumuamini

Walimpinga,,wakamkasirisha m/mungu akawaadhibu. Nabii suleiman akaliuliza lile fuvu kuwa je yeye ni nani. Likasema lile fuvu kuwa yeye ndiye aliyekuwa mfalme ( kiongozi ) wa kijiji hiko.

Nabii suleiman akaliuliza lile fuvu kuwa yupo tayari amuombee kwa allah arudi tena duniani akiwa hai. Lile fuvu likauliza ikiwa atarudishwa tena duniani je atakufa tena.nabii suleiman akamjibu ndio.

Lile fuvu likamuomba nabii suleiman wasirudi kuwa hai awaache vile vile wakiwa wamekufa,,,kutokana na machungu ya mauti. Basi nabii suleiman a.s akatoka ndani ya mji ule kisha akauamrisha upepo uufukie ule mji kama ulivyokuwa mwanzo.

Maswali,,,,,,

1 Je ni ndege gani aliyepeleka ripoti kwa 
nabii suleiman juu ya mji huo?

2 Je hao watu walikuwa na watu wa zama
zipi?

3 Na mtume wao alikuwa ni nani?

Majibu,,,,,,

1 Ndege aliyepeleka habari kwa nabii suleiman a.s juu ya mji huo alikuwa ni Kunguru.

2 Hao walikuwa ni watu wa zama za Aad,

3 Mtume wao alikuwa ni nabii Hud.

Tufikishiane elimu hii kwa ndugu zetu.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s