AMSHITAKI MKEWE KWA KUMZALIA WATOTO WENYE SURA MBAYA.

Image

Gazeti la mtandaoni la KINEDA limeripoti habari yenye msisimko wa kipekee, ambapo mwanaume mmoja aitwaye Jian Feng, amemshitaki mkewe kwa kumzaliwa watoto wenye sura mbaya.

Bwana Feng anasema alimuoa mkewe kwa furaha na upendo, lakini furaha hiyo imetoweka na kuwasababishia mfarakano wa kindoa baada ya mkewe huyo kumzalia watoto wenye sura mbaya kiasi hata cha kuwaogopa.

Kwa kujitazama utanashati wake, pamoja na urembo wa mkewe, bwana Feng hakuamini kama watoto wale wangekuwa ni wa kwake, hivyo alimshutumu mkewe kwa kukosa uaminifu katika ndoa. Lakini hata hivyo, vipimo vya DNA vilithibitisha kuwa watoto wale ni wa kwake.

Kwa bahati, baadaye mke wa Feng, alikuja kukikiri wazi na kuthibitisha kwamba, huko nyuma kabla hawajafunga ndoa, alipata kutumia kiasi cha dola $100,000 (€77,000) kufanyiwa upasuaji nchini Korea Kusini wa kujibadili mwonekano wake (Cosmetic surgery).

Kufuatia kukiri huko, Feng alimshitaki mkewe kwa kosa la kugushi mwonekano, na kutosema kweli juu ya upasuaji aliofanya kiasi cha kupelekea aonekane mrembo kinyume na uhalisia. Jaji alikubaliana na malalamiko ya Feng, na kumtakama mke alipe fidia ya dola $120,000 (€102900).

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s