YAJUE MAJINA YA MALAIKA NA KAZI ZAO(3)

MUNKAR NA NAKIIR.

(6).MUNKAR NA NAKIIR.

Munkar na Nakiir ni Malaika wawili ambao amewataja Mtume SAW. katika Hadithi sahihi kuwa ni Malaika waliowakilishwa kuuliza watu maswali kaburini. Nao wana umbo la kutisha na sauti kali sana.

Mwenyezi Mungu S.W.T. atuepushe na adhabu ya kaburi. Kila mmoja wetu baada ya kufa kwake anapozikwa kaburini mwake humwijia Malaika hawa wawili na kumuuliza maswali kama vile.

“Nani Mungu wako? Nani Mtume wako? Na nini dini yako?” Ikiwa mtu huyo hapa duniani alikuwa mtiifu kwa Mwenyezi Mungu S.W.T. na Mtume Wake S.A.W. ataweza kujibu maswali hayo kwa urahisi.

Lakini ikiwa ni kinyume ya hivyo maswali hayo yatakuwa magumu kwake, hivyo inatupasa tujitayarishe kwa maswali hayo ya kaburini. Na urahisi wa kujibu kwake inategemea na jinsi mtu alivyoishi katika maisha yake hapa duniani. Yaani mtu mwema au muovu?

(7).HARUUT NA MARUUT.

Nayo haya ni majina ya Malaika wawili aliowatuma Mwenyezi Mungu S.W.T. kwa watu wa Baabil (Babylon hivi sasa ni nchi ya Iraq) ili wawafanyie mtihani wa kuwafundisha uchawi.

Na walikuwa hawamfundishi mtu yeyote yule ila baada ya kumuonya kwao kwamba ukitaka tukufunze basi utakufuru. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Baqarah aya ya 102,

وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنْزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُر*

Na wakafuata yale waliyo zua mashet’ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet’ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru.

(9).RAQIIB NA ATIID.
Hayo ni majina ya Malaika wawili, ambao wamewakilishwa na Mwenyezi Mungu S.W.T. kwa ajili ya kuandika kauli na vitendo vya watu. Na maana ya majina haya Raqiib na Atiid ni kuwa wamehudhuria, mashahidi kwa vile daima hawaachani wako pamoja na watu ila kwa baadhi ya mambo fulani, kama vile mtu akiwa na janaba au akiwa uchi au akiingia msalani (chooni). Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Qaaf aya ya 17 na ya 18, “_

إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ
Wanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na kushotoni.

مَا يَلْفِظُ مِنْ قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ
Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari(kuandika).

Wabillah Taufiiq.

MWISHO

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s