YAJUE MAJINA YA MALAIKA NA KAZI ZAO(2)

malaika

(2). MIKAIIL.
Mikaiil ni Malaika mwingine mwenye daraja ya juu mbele ya Mwenyezi Mungu S W T kama alivyomtaja katika Suratil Baqarah aya ya 98.

مَنْ كَانَ عَدُوًّا لِلَّهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّهَ عَدُوٌّ لِلْكَافِرِينَ.
Aliye kuwa adui wa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake na Jibril na Mikail, basi hakika Mwenyezi Mungu ni adui wa makafiri.

Naye amewakilishwa kwa ajili ya mvua na mimea kwa amri ya Mola wake. Mwenyezi Mungu S. W. T. kasema katika Suratil A‘ araaf aya ya 57

وَهُوَ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا أَقَلَّتْ سَحَابًا ثِقَالًا سُقْنَاهُ لِبَلَدٍ مَيِّتٍ فَأَنْزَلْنَا بِهِ الْمَاءَ فَأَخْرَجْنَا بِهِ مِنْ كُلِّ الثَّمَرَاتِ ۚ كَذَٰلِكَ نُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ
Na Yeye ndiye anaye peleka pepo (za kuvuma) kuwa ni bishara kabla ya kufika rehema yake. Hata hizo pepo zinapo beba mawingu mazito tunayachunga mpaka kwenye nchi iliyo kufa. Kisha tunateremsha kwayo maji, ndio kama hivyo tukatolesha kila aina ya matunda. Basi hali kadhaalika tunavyo wafufua wafu, ili mpate kukumbuka.

(3).ISRAFIIL.
Israfiil ni jina la Malaika ambaye atakayepuliza baragumu siku ya Kiyama. Naye ni mmoja wa Malaika ambaye aliyekuwa akitajwa sana na Mtume wetu S.A.W. katika dua yake kila anapoamka usiku kuabudu.

Alikuwa Mtume S.A.W. anamtaja yeye pamoja na Jibril na Mikaiil, kasema katika Hadithi iliyopokelewa na Aisha R.A.A.H. na iliyotolewa na Abu Daud.

Ewe Mwenyezi Mungu! Mola wa Jibril na Mikaiil na lsrafiil Wewe Ndiye unayehukumu baina ya waja Wako katika yale waliokuwa wakikhitilatiana, niongoze kwendea haki katika yale waliokhitilafiana kwa idhini Yako, unamuongoza umtakae kwendea
njia iliyonyooka.

(4).MAALIK.
Maalik ni jina la Malaika mkubwa wa Malaika walio walinzi wa Motoni. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Surat Zzukhruf aya ya 77,

وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ ۖ قَالَ إِنَّكُمْ مَاكِثُونَ

Nao watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi! Naye aseme: Hakika nyinyi mtakaa humo humo!

(5).RIDHWAAN.
Ridhwaan ni jina la Malaika ambae kazi yake ni mlinzi wa Peponi. Mwanachuoni Ibn Kathiir kasema, “Na mlinzi wa Peponi ni Malaika anaeitwa Ridhwaan, ameitwa (kwa jina) Musarrihan katika baadhi ya Hadithi.”

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s