YAJUE MAJINA YA MALAIKA NA KAZI ZAO(1)

Malaika

Uislamu umejengwa katika nguzo sita za lmani na nguzo tano za Kiislamu. Na moja katika nguzo za Imani ni kuamini kuwepo kwa Malaika. Na lmani yake ni faridha (lazima) kwa sababu ni nguzo ya pili katika nguzo sita za Imani.

Kuamini vinginevyo au kutokuamini ni katika maasi na kufuru na kunamtoa mtu katika mila za Uislamu. Na hata Mwenyezi Mungu S. W. T ametusisitizia katika Aya nyingi katika Qur-aani kasema katika Suratil Baqarah aya ya 177,

لَيْسَ الْبِرَّ أَنْ تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ.

Sio wema(tu huo peke yake) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi(katika kusali). Bali wema(hasa) ni wa (yule) anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii.

Mwenyezi Mungu S.W.T. kajaalia kila kitu alichokiumba kina jina lake maalum ili iwe ni alama yake ya kutambulikana kwake. Na kama vile kila mwanaadamu analo jina lake basi ni hivyo hivyo kwa Malaika.

kila Malaika ana jina lake, lafudhi ya majina yao hayafanani na lafudhi ya majina ya kibinaadamu, yaani wao hawana majina kama Athmani, au Ramadhani na Mariam kadhalika na hii inawezekana pengine ni kwa sababu wao wameumbwa si waume wala wake.

Mwenyezi Mungu S.W.T. na Mtume wake S.A.W. wametufunulia ndani ya Qur‘aani na Hadithi majina ya Malaika 12 pamoja na shughuli zao, kama ifuatavyo:

(1).JIBRIL.
Jibril ni mkubwa wa Malaika na ametajwa katika aya zaidi ya moja ndani ya Qur‘aan Kasema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Suratil Baqarah aya ya 97.

*قُلْ مَنْ كَانَ عَدُوًّا لِجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّهِ مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ.*

Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur’ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.

Jibril A.S. ni Malaika mwenye nguvu sana, na Mwenyezi Mungu S.W.T. amemsifu katika Surat Najm aya ya 5 kwa nguvu zake, kasema, “Amemfundisha (Malaika) Mwenye nguvu sana.”

Na baadhi ya Wanavyuoni wamesema kwamba,

“Jibril A.S. kwa ushujaa na nguvu zake aliweza kuiinua miji ya watu wa Luut pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake pamoja na watu wake ambao idadi yao inasemekana kuwa ni watu mia nne elfu, aliwainua mpaka mbinguni kwa kutumia bawa lake moja kati ya mabawa yake mia sita. Mbwa na majogoo walisikika sauti zao na Malaika wengine wakati wakilia; na kwa amri ya Mola wake aliiangamiza miji ile na kila kilichokuwemo humo kwa kuigeuza juu chini.”_

Mwenyezi Mungu S. W. T. kasema katika Surat Huud aya ya 82,

فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا حِجَارَةً مِنْ سِجِّيلٍ مَنْضُودٍ.

Basi ilipo fika amri yetu tuliigeuza nchi juu chini, na tukawateremshia mvua ya changarawe za udongo mgumu ulio kamatana wa Motoni,

Moja ya kazi ya Malaika huyu mwaminifu ni kupeleka wahyi kwa Mitume na Manabii wote waliotangulia. Na alimwijia mara nyingi zaidi Mtume wetu SAW.

kuliko Mitume wengine wote, kwa ajili ya kumshushia wahyi au kumfundisha baadhi ya mambo kutoka kwa Mola wake kama vile kusali na kusoma Qur‘aani.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s