BUNGE LA UJERUMANI LAIDHINISHA RASMI NDOA ZA JINSIA MOJA

Angel Merkel

Wabunge nchini Ujerumani wameidhinishwa, kwa wingi wa kura, sheria ya kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.

Wamefanya hivyos iku chache baada ya Kansela Angela Merkel kuondoa upinzani wake dhidi ya mpango huo.

Chini ya mabadiliko hayo sasa, wapenzi wanaotaka kuoana ambao awali walikubaliwa tu kuwa na ushirika, hadhi ya ndoa kamili na wana haki ya kuasili watoto.

Wapinzani wa Bi Merkel kisiasa walikuwa wanaunga mkono sana hatua hiyo.

Lakini kansela huyo, ambaye alionekana kuunga mkono kufanyika kwa kura hiyo Jumatatu, alipiga kura ya kupinga.

Mswada huo uliungwa mkono na wabunge 393, 226 wakaupinga na wanne wakasusia.

Sheria nchini Ujerumani sasa itasoma: “Ndoa inafanikishwa na watu wawili wa jinsia tofauti au jinsia moja,” shirika la habari la AFP limeripoti.

 

credits : bbc swahili

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s