KIPI CHA KUFANYA BAADA YA RAMADHANI KUONDOKA?

Mwezi mtukufu wa Ramadhani

Tumeona watu wengi wakihudhuria misikitini, misikiti ikipendeza, nyumba za Allah zikipendeza, watu wameishi maisha ya kukirimiana na kuheshimiana.

Lakini ni nini baada ya Ramadhani? Baada ya Ramadhani Allah Mtukufu anasema, “Muabudu Allah Mtukufu, muabudu Mollah wako, mpaka pale mauti yakufike”.

Ibada ni jina tu lilokusanya yale yote ambayo anayaridhia Allah mtukufu na yale ambayo anayoyapenda, usijiwekee muda wa kufanya ibada, pengine mpaka Ramadhani nyingine.

Hauwezi kujua muda wako, wakati wako wa kufa ni lini, ukipata fursa ya kuamka asubuhi basi usingoje jioni, maana yake fanya kila yanayokuwa na manufaa kwako katika maisha ya Dunia na Akhera.

Endapo ukijaliwa kufika jioni basi usingoje asubuhi, fanya pia vilevile akherati na ishi ukijijua leo hii ni mzima basi kesho utakufa, kama si kesho dakika chache utakufa, jichulie kwamba muda huu wewe una afya na unasiha.

Kuna watu wengi leo hii wapo mahospitalini wana maradhi, hawakuweza kudiriki katika mfungo wa Ramadhani, hawakuweza kufanya kheri ya aina yeyote, pengine na wao walitamani kama tulivyodiriki mimi, wewe na yule lakini hawakuweza.

Wewe unayejiwekea muda kufanya ibada, utafanya ibada Ramadhani ingine itakayokuja. Je, umefunga mkataba na Allah? ili Allah asivunje mkataba akuache mpaka Rmadhani ifike? unajua lini utakufa?

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s