JE, WAJUA TOFAUTI KATI YA MAGHFIRAH (مغفرة ) NA A’FUW (عفو )?

Allah

MAGHFIRAH : Ni vile Allah (s.w) kukusamehe dhambi zako juu ya makosa fulani ila bado makosa hayo yatabaki kuoredheshwa katika buku la matendo yako na siku ya hukumu yatakuwemo katika rikodi yako na Allah atakuuliza juu ya makosa hayo.

-Lakini hatakuadhibu kwa sababu ya makosa hayo uliyokwisha yaombea MAGHFIRAH.

A’FUW : Ni vile Allah (s.w) kukusamehe dhambi za makosa Yako na kisha kufutwa kabisa makosa hayo katika buku la matendo yako, kama vile hayo makosa hayakuwahi kutokea.

-Yatafutwa kabisa katika rikodi yako na Allah hatakuuliza kuhusu makosa hayo siku ya hukumu.

kwa sababu hiyo ndio maana mtume (s.a.w) amesema, “Dua hii ni bora zaidi kuisoma siku ya Laylatul Qadr:

Nayo ni :

“Allahumma innaka a’fuwwun tuhibbul a’fwa faa’fu ‘anniy” (Ahmad, Ibn Majah, na Tirmidhiy)”
Maana ya maneno hayo ni:

(Ya Allah hakika yako ni msamehevu na unapenda kusamehe na mimi nisamehe)

Msamaha unaoutaka hapo ni ule wa kufutiwa kabisa dhambi na makosa yako katika rikodi ya matendo yako.

-Kwa hiyo hakikisha unaisoma dua hiyo kila muda na ifanye ni miongoni mwa nyiradi zako.

ZAWADI NYENGINE MUHIMU YA KUCHUKUA

Hebu Jaalia katika fikra zako imefika siku ya hukumu na imefika zamu yako ya kuhisabiwa wala huna uhakika ya kuwa utaipata pepo ya Allah (s.w).

Mara unakuta katika rikodi yako ya matendo kuna milima kwa milima ya Wema (uliyozawadiwa) Unadhani itakuaje hapo?

Je. unajua zawadi hizo zinatoka wapi?

Ni kwa sababu katika duniya ulikithirisha kusema: *”SubhanAllah wa bihamdihi SubhanAllah al ‘Adhim”*

Mtume Muhammad (s.a.w) amesema, “Maneno mawili ni mepesi katika ulimi ila ni mazito katika mizani na anayapenda sana Al Rahman,
Maneno hayo ni:

سُبْحَانَ اللّهِ وَ بِحَمْدِهِ ، سُبْحَانَ
اللّهِ الْعَظِيمِ –

SubhanAllahi wa biHamdihi, Subhan-Allahi ‘l-`adhwiym – Ametakasika Allah na sifa njema zote ni zake. Ametakasika Allah alie mtukufu (mkubwa)

Je, wajua ni kiasi gani cha wema utalipwa ikiwa utasambaza taarifa hii yenye ukumbusho mzuri kwa ndugu na marafiki zako na wao wakakithirisha kusema haya maneno. *(SubhanAllah wa bihamdihi SubhanAllah Al Adhwiym)*

Utalipwa sana kwa sababu umewahimiza watu kutenda wema.

NA WEWE KUWA NI MIONGONI MWA WENYE KUHIMIZA WATU KHERI.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s