UFAHAMU UKWELI HUU UNAOFIKIRISHA

Ukweli Hakika

HAKIKA YA KWANZA:
Katika dhulma kubwa sana ya kijamii: ni FAMILIA kutafuta mke mwema kwa kijana wao mbaya wa tabia!

HAKIKA YA PILI:
Pale jamii inapolelewa kwenye kuogopa AIBU badala ya kuogopa HARAMU; usishangae kumkuta mume HASWALI lakini anamuamuru mkewe AJISTIRI!

HAKIKA YA TATU:
Mjinga si yule ASIEJUA kusoma na kuandika, mjinga ni yule ambaye ANAJUA muelekeo wa KIBLA lakini haswali!

HAKIKA YA NNE:
Mambo matatu HAYARUDI:
– maneno yakishatoka
– wakati ukishapita; na -kuaminiana kukishapotea!

HAKIKA YA TANO:
Maisha ni kama soko kubwa, unazunguka humo na UNACHUKUA unachokipenda katika vinavyouzwa, lakini kumbuka kwamba hesabu iko mbele YAKO na UTALIPIA thamani ya kila kitu ulichochukua!!

HAKIKA YA SITA:
Wema kwa WAZAZI WAWILI ni kisa unachokiandika wewe na watakuhadithia WATOTO wako.

HAKIKA YA SABA :
Katika adabu, ni kutomuuliza yeyote kuhusu jambo analokuficha, kwani kama hulijui basi aghlabu ni kwamba halikuhusu.

HAKIKA YA NANE:
Mauti HAYATANGOJA istikama YAKO, kuwa MUSTAKIMU, kisha ngojea mauti yako.

HAKIKA YA TISA:
BUBU anatamani kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu, KIZIWI anatamani kukisikia na KIPOFU anatamani kukiona,  lakini sisi wenye maumbile YALIYOTIMIA, TUMEANGAMIZWA na simu zetu.

HAKIKA YA KUMI:
Kuna baadhi wanaamini kwamba jicho lina HAKI, wanaamini zaidi hivyo kuliko imani yao kwamba Mwenyezi Mungu ni M’BORA wa kuhifadhi.

TUAMRISHANE MEMA.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s