GARI LAGONGA WATU NA KUUWA MMOJA KARIBU NA MSIKITI LONDON UINGEREZA

LONDON

Mtu mmoja ameuawa na wengine wanane kujeruhiwa baada ya gari kugonga umati wa watu waliokuwa wakitembea karibu na msikiti kaskazini mwa London.

Mwanamume mmoja wa umri wa miaka 48 alikamatwa kufuati kisa hicho.

Polisi wa kupambana na ugaidi wako eneo hilo. Polisi wamelielezea tukio hilo kama la kigaidi.

Waziri mkuu Theresa May amekitaja kuwa kisa kibaya akisema kuwa fikra zake ziko kwa wale waliojeruhiwa, wapendwa wao na watoa huduma za dharura eneo hilo.

Baraza Kuu la Waislamu nchini Uingereza limesema kuwa walengwa wa tukio hilo walikuwa ni waumini, huku majeruhi wengi wakiaminika kuwa ni wale waliokuwa wamemaliza tu kuswali swala ya jioni baada ya kuumaliza mfungo wa siku wa Ramadhan.

Habari na Picha kwa hisani : BBC Swahili

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s