MFAHAMU MOHAMED ADEN – BINGWA WA KUSOMA QURAN AFRIKA

Mohamed Abdullah Aden

Mohamed Abdullah Aden akisoma aya ya quran mbele ya umati mkubwa uliojitokeza Uwanja wa Taifa

Kijana Mohamed Abdullah Aden kutoka Somalia ndiye ameibuka mshindi wa mashindano makubwa Afrika ya kusoma na kuhifadhi Qur-an juzuu 30 Kati ya washiriki 17 kutoka nchi 15 Barani Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa Dar es salaam, Tanzania.

Amekabidhiwa hundi ya Shilingi Milioni 15 kutoka Amana Bank, halikadhalika amepewa cheti cha ushindi, Ipod na kuchagua kwenda nchi yeyote duniani, kijana huyo wa miaka 12 ametoa wito kwa vijana kujibidisha Katika kusoma Qur-an.

Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi Mohamed Abdullah Aden, akishuhudiwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi

Mashindano hayo ya 18 yaliyo andaliwa na Taasisi ya Al-hikma Foundation yamehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa.

Wageni wengi mashuhuri ni pamoja na Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeiry, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda, Skeikh Mkuu Dar es salaam Alhad Mussa Salum, Rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi Sambamba na ujumbe Maalumu kutoka nchini Saudi arabia.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s