KABURI LA MAAJABU LA KIYEYEU – UCHAWI ULIPOISHINDA SAYANSI (2)

Kaburi la Marehemu Martin Kiyeyeu kabla ya kuhamishwa

Kaburi la Martin Kiyeyeu kabla ya kuhamishwa

Inaendelea Sehemu ya pili(2)

Imedaiwa kuwa Tanesco walifanya mazungumzo na ndugu wa marehemu huyo ili wakubali kusogeza ama kuhamisha kaburi hilo ili kupisha zoezi la kuweka nguzo za umeme ili kupitisha umeme mahala hapo.​

Imeelezwa baadhi ya ndugu hao walikubali baada ya mazungumzo hayo na kuwaruhusu Tanesco kuhamisha kaburi hilo, lakini zoezi la kuhamisha lilishindikana na walipojaribu kulibomoa hata nyundo haikuweza kufua dafu kubomoa hata sehemu ya tofali lililojenga kaburi hilo.​

Martin Kiyeyeu

Ukiangalia kwa makini picha hii utaweza kuona jinsi nyaya za umeme wa Tanesco zilivyokwepa kaburi la Martin Kiyeyeu

Ndipo ilipoamuliwa kuweka nguzo hizo na kupitisha nyaya za umeme kiubishi.​
Lakini baada ya kumaliza zoezi hilo walishangazwa kwa kuona kuwa eneo la juu ya kaburi hilo hapakuwa ukipita umeme hali ya kuwa ulipoanzia hadi kabla na baada ya kaburi hilo umeme umejaa tele, ila eneo la juu ya kaburi hilo tu hakuna umeme.​

Jambo hilo liliwafanya Tanesco kukubali matokeo na kuamua kuchukua uamuzi wa busara kwa kuhamishia baadhi ya nguzo hizo upande wa pili wa barabara ili kukwepa eneo hilo, hivyo nyaya hizo zikavuka barabara kabla ya kufikia kaburi hilo.

Baada ya kulivuka kaburi hili, na baada ya kufanya hivyo ummeme huo uliwaka na hadi hii leo unaendelea kuwaka, hivyo Serikali japo haiamini uchawi lakini hapa iliamini uchawi upo.  

Moja ya maajabu ya kaburi hilo ni kushindwa kupitishwa kwa umeme kupita juu ya yake na pia linadaiwa kushindikana kuondolewa mara mbili na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyeuawa kwa nyuki na mwingine kufariki ghafla akiendesha tingatinga alipokuwa akijaribu kuling’oa.

Hata hivyo kaburi hilo na mengine 21 yaliyokuwa kwenye eneo hilo yaliondolewa na kuhamishiwa upande wa pili wa barabara, ambako kulikuwa na kaburi moja la mtoto wa kike wa Kiyeyeu, ambaye hakuzikwa katika eneo lililokuwa na makaburi ya ndugu zake baada ya mila na matambiko kufanyika.

Dokta Aloyce L. Kiyeyeu ni mjukuu wa marehemu Martin Kiyeyeu ambaye amerithi  taaluma ya uganga kutoka kwa babu yake, anapatikana kwa namba : 0783 83 70 93.

Mwisho

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s