KABURI LA MAAJABU LA KIYEYEU – UCHAWI ULIPOISHINDA SAYANSI (1)

Hili ndilo kaburi la MZEE MARTIN KIYEYEU aliyefariki mwaka 1974, lililoko kando ya barabara ya Iringa-Mbeya katika kijiji cha Tanangozi, Iringa Vijijini

Kaburi la Mzee Martin Kiyeyeu aliyefariki mwaka 1974, kama linavyoonekana katika picha kando ya barabara ya Iringa-Mbeya

Mpenzi msomaji uliwahi kusikia maajabu ya Kaburi hili la mtu maarufu katika fani ya waganga wa jadi Almaarufu Kiyeyeu?

Kaburi la Kiyeyeu, lipo Njiapanda ya Mlolo pembezoni kabisa mwa barabara iendayo Mkoani Mbeya ukitokea Iringa lipo upande wako wa kulia, katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.​

Hili ni kaburi alilozikwa mtu mmoja aliyekuwa Mganga maarufu wa jadi katika ukanda mzima wa maeneo ya mkoa huo, ambaye alifariki dunia miaka ya nyuma kidogo lakini hadi leo hii kaburi hilo ukiliona ni kama limejengwa jana.

Baada ya kufariki dunia mganga huyu, alizikwa kwa kufuata taratibu na mira za Machifu ambapo alizikwa kwa kusindikizwa na mtu aliye hai, aliyejitolea kwa ajili ya kuzikwa naye akiwa hai ili kumsindikiza, ambapo inadaiwa mtu huyo aliketi na kumpakata mganga huyo aliyezikwa huku akiwa amekaa.

Kaburi hilo limekuwa liwashangaza watu waliowengi na hata ndugu wa marehemu huyo kutokana na kuwa na maajabu na miujiza isiyoisha kana kwamba mtu huyo amezikwa mahala hapo jana.​

Moja kati ya maajabu makubwa yaliyowahi kutokea mahala lilipo kaburi hilo ni wakati Shirika la umeme lilipokuwa katika zoezi la kuweka Nguzo za umeme pembezoni mwa barabara hiyo na kutokana na kaburi hilo kuwa karibu kabisa na barabara kubwa.

Itaendelea Sehemu ya pili, endelea kutembelea blogu ya ASILI ZETU uweze kujifunza mambo mbalimbali kupitia makala, mafundisho ya dini, tiba za kisunnah n.k

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s