MAKOSA 8 YANAYOFANYIKA WAKATI WA SWAUMU(3)

Ramadhan Iftar

Kushindwa kutumia Mswaki wa Mti

Kosa jingine linatendeka kimazoea kuhusiana na swaumu ni imani ya baadhi ya watu ya kutotumia mswaki wa mti wakati wa mchana na wanawapinga wale wanaofanya hivyo.

Wanatoa hoja kuwa harufu ya kinywa cha mtu aliyefunga huondoshwa na mswaki huo wa mti ilihali Mwenyezi Mungu huipenda zaidi harufu hiyo kuliko harufu ya miski.

Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema, Naapa kwa Yule ambaye Mkononi Mwake ipo roho yangu, harufu itokayo kinywani mwa mtu aliyefunga ni bora kwa Mwenyezi Mungu kuliko harufu ya miski.€ (Bukhari na Muslim).

Imam Ash-Shawkaanii kairejea hadith hii pale alipozungumzia tofauti ya rai kuhusiana na iwapo harufu ya kinywa cha mfungaji inatakiwa kuwepo katika maisha haya au katika maisha ya Akhera.

Yeye akasema, Kutokana na mabishano haya, ikasemwa kuwa utumiaji wa mswaki ni makuruhu kwa mfungaji. Kisha akaongeza, Kwa hakika inapenekezwa kwa mfungaji kutumia mswaki wa mti asubuhi na jioni. Hii ndiyo rai ya idadi kubwa ya wanazuoni.

Ruhusa ya kutumia mswaki wa mti pia inathibitika kwa kufuata kauli ya jumla ya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam: Lau isingelikuwa ya kwamba ningewatwisha mzigo mzito wafuasi wangu, basi ningeliwaamrisha kutumia mswaki wa mti wakati wa kila Swala.(Bukhari na Muslim).

Imam Bukhari amesema, Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, hakubagua katika hadith hii kati ya mtu aliyefunga na yule asiyefunga.

Vilevile Bukhari kasema, Inaelezwa kuwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, alikuwa akisafisha meno yake kwa mswaki wa mti wakati akiwa na swaumu, na Ibn Umar naye alikuwa akisafisha meno yake kwa mswaki wa mti katika masaa ya mwanzo na ya mwisho ya ya mchana bila kumeza mate  yake (wakati akiwa na swaumu).

  • Kujisikia Vibaya kwa sababu ya kuamka na janaba 

Baadhi hujiona kama vile wako makosani pale wanapoamka na janaba (ama kwa maingiliano ya unyumba au kutokana na ndoto).

Wasijisikie vibaya kabisa. Badala yake waoge na kufunga. Aisha kasimulia kuwa nyakati na nyakati Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, alikuwa akiamka Alfajiri na janaba kwa makutano na wakeze.

Kisha akawa anakoga na kufunga (Bukhari). Sheikh Abdul-Aziiz ibn Baaz aliwahi kuulizwa kuhusiana na swaumu ya mtu aliyeota ndoto ya jimai ndani ya Ramadhani.

Je, ndoto hii ya kujamiiana hubatilisha swaumu na je mtu huyu hutakiwa kukoga? Akajibu kuwa ndoto za jimai hazibatilishi swaumu kwa sababu hicho si kitendo cha hiyari, na kwamba kuoga ni lazima iwapo ametokwa na manii.

Inaruhusiwa kuchelewa kuoga hadi wakati wa Dhuhuri iwapo ndoto hiyo ya kutokwa na manii ilitokea baada ya Swala ya Alfajiri.

  • Kujiona tunakosea kwa kuonja vyakula

Baadhi ya wanawake huepuka kuonja vyakula kwa kuchelea kuwa kitendo hiki chaweza kubatilisha swaumu zao. Hakuna kosa kuonja vyakula maadam tu chakula hakimezwi. Ibn Abbaas, radhiyallaahu anhu, amesema, hakuna ubaya kuonja vyakula vya vyunguni (sufuriani) au vyakula vingine.(Bukhari).

NB : Ukinyoa upara usiokote madoriani
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s