MAKOSA 8 YANAYOFANYIKA WAKATI WA SWAUMU(1)

Ramadhani

Kuna makosa ambayo watu huyaona ya kawaida wakati wa Swaumu lakini yanaweza kuathiri vibaya sana swaumu zao. Tutayatazama baadhi ya makosa haya ili kila mtu ayafahamu na hivyo kuzifanya swaumu ziwe bora na kamilifu mbele ya Mwenyezi Mungu.

  • Kushindwa kuvuta maji puani wakati wa kutia udhu

Baadhi ya watu hushindwa kuvuta maji vizuri puani pale wanapotia udhu kiasi kwamba wakati mwingine wanaishia kuosha kingo tu za pua.

Hii si Sunna ya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam ambaye amesema, yeyote anayetia udhu avute maji puani na kuyapenga nje.

Hadith hiyo ilisimuliwa na Bukhari ambaye aliongeza, Mtume swallallahu alayhi wa sallam, hakumtofautisha mtu aliyefunga na yule asiyefunga katika suala hili la kuvuta maji puani.

Hata hivyo, mtu aliyefunga ametakiwa kutozidisha mno jambo hilo. zidisheni kuvuta maji puani isipokuwa pale mnapofunga. € Imam As-Sanaa aannii amesema:

Hadith hii ni uthibitisho wa kuzidisha (kitendo cha) kuvuta maji puani wakati mtu anapokuwa hakufunga. Kuzidisha huko hakuruhusiwi wakati mtu akiwa amefunga iwapo maji yanateremkia kooni na hivyo kubatilisha Swaumu.

  • Kushindwa kuachia kula na kunywa pale Muadhini anapotoa adhana ya Alfajir

Baadhi ya watu huendelea kula na kunywa hata baada ya Muadhini kuanza kutoa adhana ya Swala. Pale wanaponasihiwa husema eti inajuzu kula na kunywa  hadi muadhini aseme Hayya ‘alal falaah” kwamba hapa ndipo wao wanapoanzia swaumu yao.

Rai hii yaweza kuwa sahihi iwapo tu kuna dalili yenye nguvu kutoka kwenye Quraan au Hadith (Sunnah) sahihi. Ingawaje hakuna dalili yoyote katika Vyanzo hivi, bado jambo hili limekuwa mazoea kwa watu wengi.

Mazoea haya yasiyo sahihi yanapingana na Hadith ambapo Mtume, swallallahun alayhi wa sallam, anasema, yeyote anayezusha jambo katika jambo letu (Uislamu), basi hilo si sehemu yake nalo litakataliwa. (Al-Bukhari). Kauli nyingine katika Muslim inasomeka:

Yule anayefanya jambo ambalo jambo letu (dini) haliwafikiani nalo basi jambo hilo litatupiliwa mbali. Isitoshe, Quraan na sunna vinabainisha wazi kuwa imsaak (muda wa kujizuia kula, kunywa na kufanya jimai) huanza pale weupe wa alfajiri unapokuwa tofauti na weusi wa usiku.

Inapofika hapo, mtu lazima aache kula na kunywa. Mwenyezi Mungu anasema, Na kuleni na kunyweni mpaka mpaka ubainike kwenu weupe  wa Alfajiri katika weusi wa usiku. (2:187). Aisha, radhiyallaahu ‘anhu,, alikuwa na kawaida ya kutoa adhana usiku.

Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia:  endelea kula vyakula vyako mpaka Ibn Makhtuum atoe adhana, kwani yeye huwa hatoi adhana mpaka kuche.€ (Al-Bukhari). Ibn Maktuum alikuwa kipofu ambaye hakutoa adhana hadi pale alipoambiwa muda tayari.

Aya na Hadith iliyotangulia vinabainisha wazi kuwa muda wa kuanza swaumu (imsaak) uanzie Alfajiri na kwamba adhana ndiyo ishara yake. Kwa sababu hiyo basi, muda wa kuanza swaumu huanza punde tu Muadhini anapoanza kutoa adhana ya swala, na sio pale asemapo Hayaâala; falaah.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s