MAKOSA 8 YANAYOFANYIKA WAKATI WA SWAUMU (2)

Ramadhan Kareem

  • Kula daku mapema mno

Kula daku mapema mno ni kosa jingine ambalo watu wamezoea kulifanya. Mtu anayekula daku mapema sana anakosa fursa ya kupata baraka na malipo makubwa yanayopatikana kwa kula daku katika wakati wake muwafaka.

Kila Muislamu lazima afuate nyayo za mtume, swallallahu alayhi wa sallam, kwa kukawiza daku. Anas, radhialaahu €anhu, kasimulia kutoka kwa Zaid ibn Thaabit ambaye alisema, tulikula daku na Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, kisha tukaswali.

Mimi nikauliza, kuna kitambo gani baina ya muda wa daku na adhana? Akajibu, kitambo chake ni kile cha kutosha kusoma aya hamsini za Quran. (Al-Bukhari na Muslim).

  • Kukawiza Adhana ya Magharibi

Kosa jingine ambalo watu wamezoea kulitenda ni kwamba baadhi ya waadhini hutoa adhana ya swala ya Magharibi pale usiku unapokuwa umeingia kabisa.

Wanadai kuwa lazima wafanye hivyo ili kuwa na uhakika, na hivyo, huikawiza adhana muda mrefu baada ya jua kuzama.

Mazoea haya yanapingana na mafundisho ya Uislamu ambayo yanasema kuwa adhana ya Swala lazima itolewe punde tu jua linapozama.

Mwenyezi Mungu anasema, Kisha timizeni Saumu mpaka usiku.†(2:187)  Mwenyezi Mungu, subhaanahu wataala kaamrisha kuwa funga ifunguliwe punde tu usiku unapoanza, hiyo ni pale jua linazama kikamilifu.

Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema, usiku unapoingia upande huu na mchana unapotoweka upande ule na jua kuzama, basi mfungaji afungue swaumu.

  • Kuchelewesha futari

Kosa jingine ambalo watu wamezoea kulitenda ni lile la kuchelewesha futari. Yapo mambo mawili yanayopaswa kuelezwa kuhusiana na jambo hili.

Kwanza, kuchelewesha futari kwaweza kupelekea kukawiza swala ya magharibi, au kuikosa kabisa, jambo ambalo ni baya zaidi. Kwa sababu hiyo, Muislamu lazima afungue swaumu yake katika muda sahihi ili kuipwahii jamaa Msikitini.

Pili, kuchelewesha futari kunapingana na Sunna ya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, na kunafungamana na kufuata nyayo za wayahudi na Manasara. Sahi ibn Sad kasimulia kuwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema,

Watu wataendelea kufanikiwa muda wa kuwa wanaharakisha kufungua swaumu.(Bukhari na Muslim) Aidha, Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema, Wafuasi wangu watabakia katika Sunna yangu muda wa kuwa hawangojei nyota zitoke wafunguapo swaumu zao.(Ibn Hibbaan).

Abu Hurayrah naye pia kasimulia kuwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema, dini yetu itaendelea kushika hatamu muda wa kuwa watu wanaharakisha kufungua swaumu zao; Mayahudi na Manaswara hukawia kufungua swaumu. (Abu Dawuud na ibn Hibbaan).

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s