TANZIA : BILIONEA ‘IVAN THE DON’ AFARIKI DUNIA

Ivan Don

“Kullu nafsin zaiqatul maut”, huu ni msemo wa kiarabu ukiwa na maana ya kila nafsi itaonja mauti, ama kwa hakika mauti tumeumbiwa wanadamu na hakuna anaeweza kuepuka kifo.

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

  كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَما الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ مَتَاعُ الْغُرُور

((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-‘Imraan: 185]

Mfanyabiashara maarufu Raia wa Uganda ‘Ivan Semwanga’ amefariki Dunia nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya shinikizo la damu.

Marehemu Ivan alikuwa miongoni mwa wadau wakubwa wa blogu ya ASILI ZETU, halikadhalika hatoweza kusahaulika kwa roho yake nzuri ya kusaidia yatima, watoto wanaoishi katika mazingira magumu na masikini kwa ujumla.

Kamwe hatuwezi kuthubutu kumlaumu Mwenyezi Mungu Subhaanah Allah kwa maana tunaamini yeye ndio aliyemleta kwenye ardhi yake tukufu na ameamua kumchukua kama vile kwa watu wengine.

Ivan ameacha watoto wa tatu wa kiume ambao walikuwa wakimtazama kama nguzo yao, inshallah Mwenyezi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s