MFAHAMU KIUNDANI JINI CHEKETU – JINI ANAYEPENDWA SANA NA MAJINI, WACHAWI NA WANGA(1)

jinn

Huyu ni miongoni mwa mashetani hatari kabisa wanaotumiwa na kupendwa sana na wanga,  jini huyu muasi hutumiwa na wanga kwa kutumwa kwa mtu fulani ili amsababishie mambo yake yawe magumu.

Pia huwasaidia kuwapitisha wanga katika pembe za nyumba na kuingia ndani kuwanga,  kila ukianzisha jambo linaishia njiani bila mafanikio,migogoro kwenye ndoa ni kazi ya jini huyu.

Pindi jini huyu akitumwa akuingie mwilini maisha yako yote utayaona magumu, jini huyu akikuingia heshima yako itaporomoka na utadharaulika bila sababu. Atahakikisha anashusha nyota yako ya mafanikio hata ukiwa na elimu kila unachokifanya atakiharibu ili mradi uonekane hufai.

Halikadhalika ukiwa na jini huyu, wewe utakuwa ni jumba la maradhi  kwani ukiumwa ugonjwa huu ukijitibu mara unakuja ugonjwa mwingine,  yaani ili mradi kila siku magonjwa tofauti tofauti.

 Yote hayo jini huyu anaona hayatoshi ushenzi mkubwa zaidi anaoufanya ni pale wachawi wake wanapokwenda kwa mtu kumuwangia yeye huwageuza sura na kumuweka mmojawapo sura inayofanana na yako.

Ili wale wanaowangiwa wakuone kama kwamba wewe ndiye mchawi kumbe maskini huna hata unalolijua ila tuu ni mchezo wa jini huyu ili akutie ubayani. Jini huyu mshenzi hushirikiana na wanga katika kukupiga chale za wanga ambazo huwa ni kama alama zao popote uendapo.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s