UFAHAMU MTI ULIOGOMA KUNG’OKA JIJINI MWANZA

Habari za muda mpenzi msomaji wa blogu ya ASILI ZETU, bila shaka ni wazima wa afya na mnaendelea na majukumu ya kusukuma gurudumu la Maisha.

Kufuatia kupata habari za mti uliogoma kung’oka jijini Mwanza ambao upo eneo la Pasiasi nikaona sina budi kuwasiliana na Ostadh Nguvumali kuweza kujua zaidi.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio, walidai kwamba mti huo ulikuwa unang’olewa upisha upanuzi wa barabara, lakini licha ya mashine za kisasa na zenye nguvu kutumika zilishindwa kuvua dafu.

“Yani Doza ilipofanya kazi kuanzia hapo juu, ilipofika tuu hapa na kuugusa tu, ile kuugusa tu ukatoa damu, wakaacha kwanza, hawakuamini hicho kitendo wakaona kawaida, then wakarudia tena, ukatoa tena damu”, alisema shuhuda mmoja

Ostadh Nguvumali alisema kwamba, ipo miti mingi ambayo imekuwa ikitumika kwenye matambiko mbalimbali ya kimila, watabibu kama vile waganga, halikadhalika miti hiyo huwa inauwezo wa kuongea na wahusika wenye mahitaji au shida.

“Ipo miti kama vile mibuyu, mizaituni au mikaratusi ambayo imekuwa ikitumika kwenye matambiko kwa kipindi kirefu tangu enzi za mababu, ina uwezo wa kuzungumza na kuwatatulia wanadamu shida zao”, alisema Ostadh Nguvumali

“Ndio maana tunashauriwa hata wakati mtu unakuwa umebanwa na haja kubwa au ndogo na ukajikuta upo mazingira ya porini, ni vyema kuanza kwa kufungua kwa dua sehemu unayotaka kujisaidia, huenda ukajisaidia sehemu ambayo mizimu ndipo inapumzika na ukajikuta umeondoka na nuksi”

Ostadh Nguvumali anapatikana kwa simu namba : 0655 46 04 56

 

-Video kwa hisani ya Millard Ayo

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s