TAHARUKI : MKUTANO WA CUF WA MAALIM SEFU WAVAMIWA, WAANDISHI NA WANACHAMA WACHEZEA KIPIGO

mvamizi

Moja ya wafuasi waliovamia mkutano wa CUF wa Maalim Seif akiwa chini baada ya kuchezea kipondo kutoka kwa wananchi

(Imetolewa na Julius Mtatiro, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, The Civic United Front – CUF) 22 April 2017.

Ndugu zangu, Leo, Jumamosi, 22 Aprili 2017, Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Juma Mkumbi (ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa) alikuwa anazungumza na vyombo vya habari katika Hotel ya VINA iliyoko Kata ya Mabibo, wilaya ya Kinondoni (jijini Dar Es Salaam), juu ya masuala mbalimbali yanayohusu wilaya yake.

Akiwa anaelekea kumaliza mazungumzo na wanahabari, ghafla, watu waliovalia KININJA/VINYAGO walipaki magari mawili karibu na hoteli na kuvamia ukumbi wa PRESS ya Mhe. Juma Mkumbi.

Wavamizi hao maarufu kama MUNGIKI, (ambao hutumwa na Prof. Lipumba) leo wakiwa na BASTOLA MOJA na MAPANGA walianza kuwapiga viongozi wa CUF akiwemo Juma Mkumbi na kuwasababishia majeraha kadhaa.

Watu waliopigwa zaidi kwenye kadhia hiyo ni waandishi wa Habari, wengi wao wameporwa simu zao na vitendea kazi mbalimbali. Hata hivyo, juhudi za wasamaria wema na wananchi wa eneo hilo zilifanyika na wananchi wakapandisha ghorofani baada ya kusikia kelele za kuomba msaada, MUNGIKI wa Lipumba wakazidiwa nguvu na kukimbilia kwenye magari yao, wakatokomea kusikojulikana.

Katika kadhia hiyo, baadhi ya MUNGIKI hao walichelewa kuwahi magari waliyokuja nayo na inasemekana walianza kukimbilia vichochoroni ambako wananchi walishakusanyika, mifukuzano ikaanza. Tunaambiwa kuwa baadhi ya MUNGIKI hao, ( akiwemo huyu pichani) wamejeruhiwa vibaya na wananchi.

The Civic United Front (CUF) tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hizo za kusikitisha, kughadhibisha na kutia aibu katika nchi yetu. Iweje leo katika nchi hii watu wavamiwe na makundi ya wahuni na kupigwa na kuumizwa? Iweje leo waandishi wa habari wazuiwe kuchukua habari za mambo muhimu ilimradi tu kuna genge la wahuni limeachwa lifanye litakavyo? Iweje leo, vyombo vya dola viendelee kulikumbatia kundi hili la Lipumba ambalo linaajita “MUNGIKI” huku likiachwa tu lijiite hivyo na kutenda hivyo.

Tukio hili la leo la Mabibo linanifanya niwakumbushe matukio mengine kadhaa ambayo MUNGIKI wa Lipumba wameyasimamia tena wakisaidia na POLISI ama wakati wa matukio hayo, au wakati wako chini ya vyombo vya Ulinzi na Usalama.

 

Credit : Jamii Forums

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s