HESHIMA YA MWANAMKE KATIKA UISLAMU(2)

heshima ya mwanamke 2

HALI YA MWANAMKE KATIKA UISLAMU

Baada ya mwanamke kuishi katika dhulma kwa muda mrefu, bila ya kupata haki zake. Allah (Subhaanahu wa Taala) alimtumiliza Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) kuja kumkomboa mwanamke na dhulma na udhalilifu alikuwa akipata kutoka katika jamii anayo ishi.

Dini ya Kiislamu inamtukuza mwanamke na inampa haki zake zote katika jamii. Miongoni mwa haki hizo. Mwanamke sawa na mwanamume katika kutekeleza majukumu ya Dini,  amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى 😦مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِنْ ذَكَرٍ أَوْ أُنْثَى وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُمْ بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ) [النحل: 97]

“Wafanyaji mema, wanaume au wanawake, hali ya kuwa ni Waislamu, tutawahuisha maisha mema, na tutawapa ujira wao mkubwa kabisa”.

Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) alimfadhilisha mwanamume kuliko mwanamke katika baadhi ya mambo, kwasababu ya majukumu mazito ya mwanamume katika kusimamia familia.

Mwanamke anastahiki kurithi. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema:

وقال سبحانه) : لِلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنْهُ أَوْ كَثُرَ نَصِيبًا مَفْرُوضًا) [النساء: 7]

“Wanaume wana sehemu katika mali wanayoacha wazazi wao na jamaa walio karibu. Na wanawake pia wanayo sehemu katika yale waliyaacha wazazi wao na jamaa walio karibu. Sawa yakiwa kidogo au mengi. Ni sehemu zilizofaridhishiwa (na Mwenyezi Mungu)”.

Mwanamke ana haki ya kuchagua mume wa kumwoa,  hawezi kuolewa bila ya ridhaa yake,  kinyume na zama za jahiliyah, mwanamke alikuwa ni bidhaa na chombo cha starehe kila mtu anakichukuwa kwa thamani ndogo, na kwa lengo la kutekeleza matamanio yake.

Mwanamke ana haki ya kujikomboa kutokana na mume dhalimu. Sheria ya kiislamu imempatia mwanamke haki ya kutoa talaka kwa mwanamume mwenye tabia mbaya, mwenye kumnyima mkewe haki zake.

Haya ni baadhi ya mambo muhimu mabao mwanamke amepewa katika Dini ya kiislamu. Na hii ndio hali halisi ya mwanamke katika Uislamu. Uislamu ulimrejeshea mwanamke hadhi na utukufu wake katika jamii, na ikatambua mchango wake mkubwa katika kuandaa kizazi cha kesho na kulea viongozi wa kusimamia Dini ya kislamu.

Amesema Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) katika Hija:

“Mcheni Mwenyezi Mungu katika kuwasimamia wanawake, kwa sababu wao ni wasaidizi wenu”.

Mtume anaweka wazi cheo cha mwanamke nacho ni wasaidizi wa wanaume, sio mtumwa au mtumishi kama wanavyomdai watu wengine kwamba uislamu umemfanya mwanamke kuwa ni mtumwa hana haki yoyote katika jamii.

Enyi waja wa Allah, tumcheni Allah na tufanyeni bidii kuwasimamia wake zetu kulingana na alivyo tufundisha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s