HESHIMA YA MWANAMKE KATIKA UISLAMU(1)

Heshima ya mwanamke

Ndugu katika imani, suala la mwanamke ni suala ambalo liliwashughulisha watu wengi waliopita na linaendelea kuwashughulisha wengi katika zama zetu hizi. Dini na mila mbalimbali zimezungumzia hali ya mwanamke katika jamii.

Wasomi wa elimu na falsafa tafauti wamejaribu kuzungumzia cheo cha mwanamke katika jamii. Lakini kila kundi linajaribu kumzungumzia mwanamke kwa misingi ya kufikia malengo yao.

Katika makala hii tutajaribu kuangazia cheo cha mwanamke katika jamii mbalimbali. Tutaangalia hali ya mwanamke kabla ya kuja Uislamu, na hali yake katika Uislamu, na hali yake katika mataifa ya magharibi.

HALI YA MWANAMKE KABLA YA KUJA DINI YA KIISLAMU

Alikuwa mwanamke katika zama za ujinga akionekana kama bidhaa ambayo haina thamani. Kila mtu anaweza kumiliki bidhaa hiyo wakati wowote. Wanaume wakioa wanawake bila ya idadi maulumu na kuacha bila ya idadi ya talaka.

Mwanamke haruhusiwi kumiliki chochote, hana haki ya kurithi, anaweza kuolewa na zaidi ya mume mmoja. Mwanamke hakuwa na cheo katika jamii ya ujahiliyah, bali alikuwa akionekana ni mtu anayeleta aibu katika jamii.

Ikafikia hali hiyo, baadhi ya wanaume kuwazika mabanati wao wakiwa wadogo kuogopea kuleta aibu katika jamii. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) anatueleza hali ya mwanamke Akisema:

قال تعالى 😦وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُمْ بِالْأُنْثَى ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ 58يَتَوَارَى مِنَ الْقَوْمِ مِنْ سُوءِ مَا بُشِّرَ بِهِ أَيُمْسِكُهُ عَلَى هُونٍ أَمْ يَدُسُّهُ فِي التُّرَابِ أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ ) [النحل: 59]

“Na mmoja katika wao anapopewa khabari ya kuzaliwa mtoto wa kike, unabadilika uso wake huwa mweusi na akajaa sikitiko, anajificha na watu kwa sababu ya khabari mbaya ile alioambiwa. (anafanya shauri) Je, akae naye juu ya fedheha hiyo, au amfukie udongoni, ni mbaya mno hukumu yao hiyo”.

Hii ndio hali halisi ya mwanamke kabla ya kuja Dini ya kislamu, na hali hii ilikuwa sawa katika mataifa yote, sawa taifa la kiarabu na wasiokuwa waarabu.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s