YAFAHAMU MAKAAZI YA MAJINI NA MUDA WANAOWEZA KUPATIKANA(2)

Bundi

Habari za asubuhi mpenzi msomaji wa blogu ya ASILI ZETU, bila shaka ni wazima wa afya na mnaendelea vyema baada ya wikiendi ndefu ya sikukuu za Pasaka kwa upande wa ndugu zetu wakristo.

Kwa wale wafuatiliaji wa makala hii, bila shaka mlikuwa mkiisuburia kwa hamu sehemu ya mwisho ambayo kwa rehema nilizojaliwa na Allah nimeweza kuimalizia kuandika, endelea nayo hapo chini.

Mashetani pia huishi ndani ya majumba wanayoishi watu. Mtu anaweza kuwazuia wasiingie ndani ya nyumba au anaweza kuwafukuza ndani kwa kulitaja Jina la MwenyeziMungu (Bismillah), kumdhukuru au kumtaja Allah, kusoma Qur’an hasa hasa “Ayatu Qursiyu ya Surati Baqara (ambayo ni aya ya 255 ya sura hiyo).

Mtume (saw) amesema kuwa mashetani huzagaa na kurandaranda kwa wingi pale giza linapoanza kuingia. Kwa sababu hii, amewanasihi Waislamu kuwarudisha ndani watoto wao katika muda huo. Haya yamesemwa katika Hadith iliyonakiliwa na Bukhari na Muslim.

Mashetani huikimbia Adhana na hushindwa kustahamili kuisikiliza. Katika Mwezi wa Ramadhani Mashetani hufungwa minyororo (pingu).

             MAHALI WANAPOPENDA KUKAA AU KUKUSANYIKA MASHETANI

Mashetani hupendelea kukaa baina ya kivulini na juani (baina ya kivuli na mwanga wa jua). Kwa sababu hiyo, Mtume (saw) amewakataza Waislamu kukaa sehemu hizo. Hadith hii sahihi imenakiliwa katika vitabu vya Sunan na vitabu vingine.

                                          WANYAMA NA MAJINI

Katika Hadith ya Ibn Masud iliyonakiliwa katika Sahih Muslim, Majini walimuuliza Mtume (saw) kuhusu chakula chao. Akawaambia, “kila mfupa uliosomewa Jina la Allah ni chakula chenu.

Muda uleule mfupa utakapofika mikononi mwenu utavikwa nyama. Na kinyesi ( cha ngamia) ni chakula cha wanyama wenu.” Hivyo, Mtume (saw) katujuza kuwa majini wanao wanyama wao ambao chakula chao ni kinyesi cha wanyama wa binadamu.

          WANYAMA MAALUM AMBAO MASHETANI HUANDAMANA NAO

Mashetani huandamana na wanyama kadha wa kadha kama vile ngamia. Mtume (saw) kasema:

“Kwa hakika ngamia kaumbwa kutokana na mashetani. Na nyuma ya kila ngamia yupo shetani.”1 Kwa sababu hiyo, Mtume (saw) katukataza kusalia kwenye mazizi ya ngamia. Imenakiliwa Hadith katika Vitabu vya Musnad Ahmad na Sunan Abu Dawud kuwa Mtume (saw) amesema:

“Msiswalie katika mazizi ya ngamia, kwani wanatokana na mashetani. Ila swalieni kwenye machungio ya kondoo kwani wana bar-ka.”2 Ibn Majah,
katika Kitabu chake, Sunan, kanakili Hadith yenye isinadi sahihi kuwa Mtume amesema:

“Msiswalie mahali wanapopumzikia ngamia (yaani pale waendapo baada ya kunyweshwa maji), kwani wao wameumbwa kutokana na mashetani.”

Hadith hii inakanusha madai ya wale wanaosema kuwa sababu ya kukatazwa kusalia kwenye mazizi ya ngamia ni kuwa mkojo na kinyesi chao ni najisi. Ukweli ni kuwa mkojo na kinyesi cha mnyama yeyote yule anambaye ni halali kuliwa hakihesabiwi kuwa ni najisi.

Wale wanaosumbuliwa na mashetani wa kijini, ndoto mbaya, maruhani, pete ya bahati, kusafisha nyota, mvuto wa biashara n.k. Wasiliana na Ostadh Kitengula : 0755 34 63 08

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s