FAHAMU UMUHIMU WA MBEGU ZA TIKITI MWILINI

Tikitimaji

Ni vema kwenye mlo tukapendelea kuweka na matunda kwa sababu ya kuongeza madini mbalimbali yanayopatikana katika lishe.

 Tikitimaji ni moja ya matunda yao. Wakati tukifurahia utamu, unyororo na ladha ya matunda mara nyingi tumekuwa tukiondoa mbegu bila kujua faida za mbegu hizo katika afya.

Mbegu za tikitimaji pia zinajulikana kwa jina la Mbegu za Kalahari; zanawezo kukupatia virutubisho lishe kama vile Mafuta, protini, madini na Vitamini B.

Mbegu ya tikiti inasaidia katika uzalishaji wa melanin, rangi ambayo husaidia katika ngozi na nywele.

Aidha mbegu hizo utumika kuwa supu, kupamba salad na kufanya vitafunio,  mbegu za tikitimaji pia zimekuwa zikitumika katika matibabu ya ugonjwa wa kisukari.

Hii inahusisha kuchemsha mbegu za tikitimaji katika lita moja ya maji kwa muda wa dakika 45, kisha kunywa kwa kuchanganya na supu.

Mbegu hii pia inamanufaa katika kulinda mwili na kama vile haitoshi ulaji wa kalori au protini ambazo zinapatikana katika mbegu hizo zinaweza kuimarisha hali ya kusababisha ugonjwa wa utapiamlo na kwashakoo.

Uwepo wa fati katika mbegu hizo kutunza ngozi kiafya, kuwa nyororo, laini, imara na nzuri zaidi ikiwa ni pamoja na kuwa msaada wa kuzuia ugonjwa wa ngozi.

Vitamin B pia ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha mishipa ya damu, mfumo wa neva na mfumo wa kinga ya afya, wakati huohuo Mbegu za tikitimaji nichanzo kizuri cha kalori chanya na nishati na ina ufanisi katika kumbukumbu.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s