CAMEROON MABINGWA WA AFRIKA 2017

cameroon

Miamba ya soka barani Afrika, timu ya mpira wa miguu ya Cameroon, imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la Afrika 2017.

Cameroon imenyakua kombe hilo baada ya kuilaza timu ya taifa ya Misri katika fainali za Afcon kwa jumla ya mabao mawili kwa moja katika mchezo uliopigwa nchini Gabon.

Mchezaji wa Misri, Mohamed Elneny ndio alikuwa wa kwanza kuiandikia timu yake bao la kuongoza mnamo dakika ya 22 kabla ya Nicolas N’Koulou kusawazisha na kufanya matokeo kuwa moja moja katika angwe ya pili ya mchezo.

Nyota ilionekana kuwang’aria Cameroon, baada ya mchezaji Vicent Aboubakar ambaye alitokea benchi kuachia shuti kali lilomshinda golikipa wa Misri, Essam el hadary na kufanya mchezo umalizike kwa Cameroon 2 – 1 Misri.

Hii inakuwa mara ya tano(5) kwa timu ya Taifa ya Cameroon kutwaa kombe la Afrika, huku mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 1972, 1984, 2000,2002 na 2017.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s