WACHIMBAJI 15 WA MGODI WA MADINI WAOKOLEWA

image-1

Wachimbaji madini 15 wameokolewa wakiwa hai baada ya mgodi wao kupolomoka siku tatu zilizopita.

Ajili hiyo iliyokea usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita, tarehe 26 Januari, katika mgodi uitwao RZ Gold Mine, unaomilikiwa na raia wa China katika machimbo ya dhahabu yaliyopo Geita Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Manusura hao walionokena wadhaifu kiafya, lakini walipatiwa huduma ya kwanza mara moja na kisha kupelekwa katika kituo cha afya kilichopo jirani

Uchunguzi wa nini hasa kilisababisha ajali hiyo unaendelea, lakini hii si mara ya kwanza kwa tukio kama hili kutokea

Mwaka jana mwezi Novemba, Tanzania ilisherehekea ukoaji wa ‘kimiujiza’ baada ya wachimbaji watano kuokelewa wakiwa hai baada ya kukwama chini ya ardhi kwa siku 41.

Eneo la Magharibi mwa Tanzania lina migodi mingi na wachimbaji wengi hutoka vijiji vya jirani.

Naibu waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani, amesema serikali itahakikisha wachimbaji wana kuwa salama.

Mgodi huo utakuwa chini ya uangalizi kwa siku tano kabla wachimbaji kuruhusiwa kufanya kazi.

Naibu waziri pia amewaagiza makamishina wa madini kufanyia tathmini migodi mwingine ya wachimbaji wadogo kwa siku tano, kuanzia kesho.

Chanzo : Bbc Swahili

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s