KIPA WA KAGERA SUGAR AFARIKI DUNIA

david-burhan

Taarifa za awali, zinasema kwamba kabla ya umauti, Burhan aliugua ghafla wiki iliyopita akiwa safarini kutoka Singida na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo usiku wa Alhamis.
 
Siku ya Ijumaa alihamishiwa Hospitali ya Kagera Sugar, na kisha kusafirishwa hadi Bugando siku ya Jumapili kwa uchunguzi zaidi. Usiku wa Jumapili, alifanyiwa vipimo na kuonekana kwamba mapafu yamejaa maji. Katika jitihada za kupatiwa matibabu alifariki saa nane za usiku wa Jumapili.

Mwili wa marehemu kwa sasa uko Bugando, na uongozi wa Timu unafanya taratibu za kusafirisha hadi nyumbani kwao Iringa.

Wakati kifo hicho kinatokea, Kagera Sugar ilikuwa kwenye maandalizi ya asilimia 100 ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kama ilivyo kwa mgeni wake Mtibwa Sugar ambako kwa mujibu wa ratiba, ulikuwa uchezwe leo Januari 30, 2017.

Mchezo huo umeendelea kwa sababu viongozi wa timu zote mbili, walikubaliana kucheza ili kumuenzi marehemu Burhan; pili maandalizi yaliyokamilika na zaidi, Mtibwa Sugar tayari ilikuwa Kagera kwa ajili ya mechi hiyo.

Pia mchezo huo umeendelea baada ya familia kutangaza kuwa mazishi ni Jumatano Februari mosi, 2017 hivyo wadau kadhaa kesho Jumanne watapata nafasi ya kusafiri kwenda Iringa, ambako wamepanga kuzika. Kanuni za Ligi Kuu, zinaahirisha mchezo kama mchezo unafanyika siku ya mazishi, lakini marehemu Burhan atazikwa Jumatano, hivyo wengi watapata fursa ya kwenda kushiriki.

Kwa sababu hizo, TFF ilibariki mchezo huo ufanyike na zaidi tumeagiza wavae vitambaa vyeusi begani na kupata dakika moja ya maombolezo. Kadhalika michezo yote ya wikiendi hii, tunaagiza wachezaji kuvaa vitambaa vyeusi na kupata dakika moja ya maombolezo kabla ya mpira kuanza.

Marehemu Burhan ni Mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pan Africa, Abdallah Burhan. Alianzia timu ya vijana wa chini ya miaka 20 ya Kagera Sugar, kabla ya kujiunga na Lipuli ya Iringa, Tanzania Prisons na Mbeya City za Mbeya, Maji Maji ya Songea na baadaye kurudi Kagera Sugar.

Mungu amlaze mahala pema.

 

Credits : Saleh Jembe

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s