IJUE TAFSIRI YA NDOTO YAKO

ndoto

Katika Uislamu tumeambiwa Ndoto ni sehemu ya unabii tulioachiwa, pia uislamu unaeleza aina kuu mbili za ndoto yaani Ndoto zinazotokana na shetani na ndoto inayotoka kwa mwenyezi mungu. 

Pia Uislamu umeeleza ndoto ya kweli uotwa muda gani (Mfano amesema bwana Mtume, ndoto yeyote atakayeota muumini kabla ya swala ya alfajiri, ndoto hiyo ni ya kweli), kwa ufupi ndoto ya kweli ni ile mtu anayeota usiku wa manane akiwa hana msongamano wa mawazo na hajalala na janaba.

Nimekuwa nikipokea ujumbe nyingi kwenye simu yangu ya kiganjani kutoka kwa watu mbalimbali wakihitaji niwatafsirie ndoto zao,  hivyo nikaona vyema niwashirikishe na nyie japo kwa uchache.

Ndoto hizi nimezitafsiri kwa mujibu wa dini yangu ya kiislam  na sio dini nyingine, japokuwa baadhi ya ndoto inabeba maana sawa kwa muislamu na asiye muislamu.  

 

NATUMBUKIZWA KISIMANI HUKU WATU WAKIWA WAMENISHIKA MIGUU NA MIKONO

Habari yako ndugu mtafsiri wa ndoto,  mara kwa mara nimekuwa nikiota watu wamenishika kichwa, miguu na mikono wakitaka kunitumbukiza katika kisima kirefu sana. Hii ndoto imekuwa ikinitesa sana,  nahitaji kujua maana yake

TAFSIRI YAKE :

Mimi ni buheri wa afya na natumaini nawe hujambo pia.  Tafsiri ya ndoto yako inaonesha ndugu au jamaa zako wanataka kukutendea uadui,  lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa wanavyotaka na utakuja kuwa na uwezo wa mali na mamlaka kuliko wao.

 

NAOTA NDEGE MKUBWA ANARUKA ALAFU NIKIMUANGALIA ANANINYEA

Shikamo Ustadh,  mimi ni mwanamke wa makamo,  naishi na mume na tumejaliwa kupata watoto,  shida niliyonayo ni kwamba nimekuwa nikimuona ndege mkubwa akiruka ndotoni lakini ghafla nikimtazama ananinyea licha ya kuwa mbali.

TAFSIRI YAKE :

Kuona ndege anaruka alafu anakunyea hiyo tafsiri yake ni Surat fil,  hapo unaonywa kuwa kuna jambo au kitu unachokifanya kilichovuka mipaka hivyo huenda ukaangamia,  acha mara moja.

 

NACHOTA  MAJI  KWENYE  KISIMA  KISICHOKUWA  NA  WATU

As-salaam alaikum Ustadh, mimi ni mdada, umri wangu ni miaka 18 nina mchumba,  nahitaji unitafsirie ndoto yangu,  naota nipo kisimani nachota maji,  hicho kisima kipo mbali na makazi ya watu.

TAFSIRI YAKE :

Wa-Alaikum-Salaam , Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote,  tafsiri ya ndoto yako ni kuhusu uhusiano wako, ndoa ipo karibu na utaolewa, hivyo fanya jitihada katika kufanya ibada na kumuomba Allah.

Ndoto ni mojawapo ya njia ambazo Mwenyezi Mungu hutumia kuongea na watu wake.  Kwa kuwa MUNGU hutumia ndoto kufikisha ujumbe wake kwetu ,Lakini pia shetani naye hutumia ndoto kufikisha maharibifu yake kwa watu wasiopenda kufanya ibada.

Kama hauoti ndoa unahitaji ufanyiwe dua maalum na kama unaota ndoto na huelewe maana ya ndoto uliyoota pia unahitaji msaada wa kutafsirwa na kupewa maana yake.

Ustadh Abdul ni mtaalam wa kutafsiri ndoto Afrika mashariki na kati, pia huwasomea kisomo watu wanaosumbuliwa na matatizo mbalimbali, anapatikana kwa simu nambari 0743 – 53 79 98.

 

 

 

 

Advertisements

2 responses to “IJUE TAFSIRI YA NDOTO YAKO

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s