TAMBUA MISINGI YA TABIA ZAKO KWA KUTUMIA ALAMA ZA NYOTA YAKO

zodiac

Unajimu au Astrolojia ni elimu juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha ya binadamu duniani.

Wanazuoni wa unajimu wanaeleza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu na matukio kama amani, vita au maafa,  mahusiano haya hayajaweza kuthibitishwa na sayansi ya fizikia au sayansi nyingine.

Alama za nyota 12 ni msingi wa falsafa hii ya unajimu,  Astrologia imekuwa ikitumika kwa miaka mingi lakini siku zote imekuwa ikipata upinzani mkubwa toka kwa wana sayansi.

Astrolojia ina misingi tokea enzi za zamani wakati sayansi ilipokuwa ya chini na imani za kiroho na kiungu zikiwa za kiwango cha juu katika jamii nyingi.

Baadhi ya tafiti zilizofanywa kuchunguza usahihi wa astrolojia unaonyesha kuna usahihi wa asilimia kama 3o tu,  hii si haba ,kuna ukweli basi katika hili japo bado kuna upinzani mkubwa toka katika ulimwengu wa sayansi ya kisasa.

TABIA ZA WATU NA ALAMA ZA NYOTA

Alama za nyota zinabashiri tabia na haiba ya binadamu katika dunia. Mpangilio au nafasi ya sayari katika mzunguko wake angani unaaminika kuleta athari kwa binadamu na matukio katika dunia.

Kuna alama 12 za kiastrolojia. Kila moja ina mvuto wa nguvu wa kipekee toka katika nyota.

Alama hizi ni kama ifuatavyo:

Samaki (Pisces):Feb 19 – Machi 20

Kondoo (Aries): Machi 21 – Aprili 19

Ng’ombe (Taurus): Aprili 20 – Mei 21

Mapacha:(Gemini ): Mei 22 – Juni 20

Kaa(Cancer): Juni 21 – Julai 22

Simba(Leo): Julai 23 – Agosti 22

Mashuke(Virgo):Agosti 23 – Sept 22

Mizani (Libra): Sept 23 – Okt 22

Ng’e (Scorpio): Okt 24- Nov 21

Mshale (Sagittarius): Nov 22- Des 21

Mbuzi(Capricorn):Des 22 – Jan 19

Ndoo (Aquarius):Jan 20 – Feb 18

Makundi ya Alama za Nyota:

Alama hizi 12 za nyota zinagawanyika katika elementi 4 zijulikanazo kama:

 • Moto:Yenye matamanio ya mafanikio au makuu,dadisi
 • Maji:Yenye kubadilika na yenye uwezo wa ufahamu wa ndani
 • Hewa:Imara na yenye kukuza au kuendeleza
 • Udongo:Yenye elimu au uwezo wa kutambua na yenye kuhamasisha

 

Hizi ni elementi nne zinazoongoza astrologia. Kila kimojawapo kinabeba tabia fulani.

Alama hizi 12 za nyota zimegawanyika kama ifuatavyo:

 • Moto: Kondoo, Simba,Mshale
 • Maji: Ng’e, Samaki, Kaa
 • Hewa: Mapacha, Mizani, Ndoo
 • Udongo: Ng’ombe,Mashuke,Mbuzi

 

Kila alama ya nyota 12 zimegawanyika pia katika makundi mengine matatu ambayo ni:

 • Yenye Umuhimu au Msingi “Cardinal”: Kondoo, Kaa,Mizani,Mbuzi
 • Yenye Kubadilika “Mutable”: Ng’ombe, Simba, Ng’e na Ndoo
 • Isiyobadilika “Fixed”: Mapacha, Mizani, Mshale na Samaki

 

Alama ambayo iko katika moto na iko katika kundi la msingi huwa na tabia za upinzani na ubishani wa hali ya juu kama Kondoo

Alama ambayo ipo katika kundi la Udongo na Kubadilika huwa na tabia za utulivu wa hali ya juu kama Ng’ombe.

Haiba na Tabia za Alama za Nyota

#1 Nyota ya Kondoo: Machi 21 – Aprili 19

alama-za-nyota_kondoo

 • Ni mwenye maamuzi yasiyopinda na mtendaji mzuri wa kazi.
 • Anategemea makuu juu yake mwenyewe na kutoka kwa wengine
 • Mwenye kujitegemea na mwenye ari ya hali ya juu
 • Anauthubutu wa kujaribu mambo makubwa
 • Mwenzilishi wa mambo na mbunifu
 • Kiongozi
 • Muongeaji
 • Ni mwenye hisia kali na asiye na uvumilivu mkubwa.
 • Mwaminifu kwa marafiki na familia
 • Anajali mpenzi wake na mwenye hisia kali za mapenzi

 #2

Nyota ya Ng’ombe: Aprili 20 -Mei 20

alama-za-nyota_ngombe

Ni alama ya udongo:

 • Ni mwenye nguvu na mstahimilivu kimwili na kiakili
 • Makini na muangalifu
 • Ana kiburi na asiyekubali kushindwa kirahisi
 • Mstahimilivu
 • Mwenye kutegemewa
 • Ni mgumu kubadilika
 • Anapenda vitu vizuri na vya thamani
 • Unapenda urembo na vitu vya kupendeza
 • Mwenye hisia zilizofichika
 • Huenda akaonekana mbinafsi lakini ni wenye kutoa wakiwa na mali au fedha.

 #3 Nyota ya Mapacha: Mei 21 – Juni 20

alama-za-nyota_mapacha

Ni alama ya hewa:

 • Ni mwenye kipaji kikubwa,mwenye kubadilika na anayechoka haraka na kukata tamaa
 • Anafikiri kwa haraka na mcheshi
 • Ni mwasilianaji mzuri
 • Ni mtu anayependa watu na mwenye kupenda mabadiliko.
 • Mwenye kuamua kwa akili na mbunifu
 • Hana utulivu
 • Ana mipango na malengo makubwa
 • Mwenye kubadilika kirahisi

#4 Nyota ya Kaa: Juni 21 – Julai 22

alama-za-nyota_kaa

Ni alama ya maji:

 • Anapenda kukaa nyumbani na kuwa na makazi mazuri yenye kumpautulivu ,usalama na amani
 • Anapenda marafiki na familia. ANanpenda kufuatilia historia ya ukoo
 • Hisia zake ni za wazi na ni rahisi kujulikana
 • Ana huruma
 • Ni mwangalifu
 • Mkimya na

 #5  Nyota ya Simba: Julai 23 – Agosti 22

alama-za-nyota_simba

Ni alama ya moto:

 • Kama alivyo simba ni jasiri na mwenye uthubutu.
 • Anapenda kuonekana na watu
 • Sanaa ni mojawapo ya maeneo ambayo anayamudu na ambayo yanamfanya afanikiwe
 • Wana maamuzi mazuri na ni waigizaji mahiri.
 • Ni wenye moyo wa kutoa na wenye upendo mkubwa
 • Ni viongozi wazuri na wenye nguvu
 • Mwenye matumaini mazuri
 • Mwenye kuheshimika
 • Mshindani
 • Mpangiliaji mzuri wa mambo ya kufanya
 • Mwenye mvuto

#6 Nyota ya Mashuke: Agosti 23 – Septemba 22

alama-za-nyota_mashuke

Ni nyota yenye alama ya udongo

 • Ana mategemeo makubwa juu yake mwenyewe na kutoka kwa watu wengine
 • Ni mwenye ujuzi na mwenye mafanikio makubwa kazini
 • Ni mchunguzi na mdadisi wa mambo na mwenye kufanya kitu kimoja kwa wakati mmoja.
 • Wapangili wazuri wa muda na watekelezaji
 • Ni mdadisi na mbishi katika kuhakikisha mambo yanafanyika kwa ukamilifu.
 • Ni wafanya kazi wenye umakini na ni waangalifu katika kazi zao.
 • Wanajali afya

#7 Nyota ya Mizani: Septemba 23 – Oktoba 22

alama-za-nyota_mizani

Ni alama ya hewa. Mwenye nyota ya mizani anatumia muda mwingi katika kuleta usawa na haki na kusuruhisha migogoro.

Mizani anatumia akili zaidi kuliko nguvu za mwili.

 • Husimamia haki na usawa
 • Anapenda sanaa na urembo
 • Wabunifu wa sanaa
 • Ni mpenzi wa muziki
 • Ni muwazi katika kuonyesha upendo
 • Ana ustadi wa kukabiliana na mambo ya kijamii
 • Anatoa matazamo wake pale tu anapochokozwa au anapoguswa kihisia
 • Mpenda amani
 • Wenye mvuto wa kupendwa

#8 Nyota ya Ng’e: Oktoba 23 – Novemba 21

alama-za-nyota_nge

Ni alama ya nyota ya maji na ni mwenye hisia nzito

 • Anapenda mambo makubwa na maisha ya mazuri
 • Mjasiriamali namwenye uwezo wa kukabiliana na vizingiti vikubwa
 • Anapenda malumbano makali
 • Wanatumia nguvu
 • Jasiri
 • Wastahimilivu
 • Washindani
 • Wanauwezo ,
 • Wachunguzi wa mambo
 • Wasiri
 • Ni mpenzi mzuri na mwenye tabia za umiliki
 • Wanajitegemea
 • Ni wenye maamuzi

#9 Nyota ya Mshale: Novemba 22 – Desemba 21

alama-za-nyota_mshale

Ni alama ya moto na ni mwenye mapenzi mazito na vitu

 • Mwanafalsafa na mkusanyaji wa habari
 • Mwenye uwezo mkubwa kiakili ma anapenda changamoto
 • Ni mwenye nguvu ambazo humfanya mara zote aende mbele.
 • Ni mwenye kupenda uhuru
 • Ni mpenzi mwenye mvuto na anapenda kumridhisha mpenzi wake
 • Rafiki
 • Mwenye ari
 • Hawana utulivu
 • Waaminifu na wakweli
 • Wanapenda safari

#10 Nyota ya Mbuzi: Desemba 22 – Januari 19

alama-za-nyota_mbuzi

Ni alama ya udongo na mwenye kuhitaji nyumba yenye amani ili kuhisi ukamilifu.

 • Mwenye malengo , mipango na matarajio makubwa
 • Ni mtatuaji wa matatizo kwa vitendo na mapangiliaji mzuri wa mambo-Mtendaji
 • Ni mwenye mipango na mfuatiliaji wa mipango yake
 • Si mshirikishaji mzuri mpaka aombwe au asukumwe.
 • Ni mpenzi mzuri na rafiki wa maisha
 • Mgumu kubadilika
 • Mbishi na asiyekubari kushindwa kirahisi
 • Mfanyabiashara
 • Mwajibikaji

#11 Nyota ya Ndoo: Januari 20 – Februari 18

alama-za-nyota_ndoo

Ni alama ya hewa:

 • Ni mbinafsi na asiyependa kufuata utaratibu au sheria.
 • Wakipekee
 • Anaejitegemea na hupenda kuwa peke yake
 • Mwenye huruma
 • Muona mbali
 • Mwenye ufahamu wa hali ya juu nma mbunifu
 • Anafanya marafiki wa aina mbalimbali
 • Ana utu na mwenye kudai haki
 • Anapendwa na watu na anategeneza urafiki kwa haraka
 • Anapenda sanaa na maisha ya anasa.

#12 Nyota ya Samaki: Februari 19 – Machi 20

alama-za-nyota_samaki

Ni alama ya maji na ni mwenye ufahamu wa hali ya juu wa mambo.

 • Ni mkweli na mwenye hisia nzito
 • Hana ubinafsi
 • Ni mpenzi mwaminifu na rafiki
 • Mpenda amani
 • Ana huruma
 • Anajitoa
 • Wana ndoto
 • Wabunifu
 • Wana aibu

 

Kama unahitaji kusafishwa nyota, kusomewa dua, mvuto wa biashara au unasumbuliwa na mapepo na mashetani, wasiliana nae kwa simu namba : 0757 47 91 43 .

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s