ZIJUE KINGA 5 DHIDI YA UCHAWI NA MAJINI

maajabu

Hakika sifa zote ni za Allah,  tunamsifu,  na tunamuomba msaada na tunamuomba maghafira,  tunamuomba atuhifadhi na shari za nafsi zetu na maovu ya matendo yetu.

Nikija kwenye safu hii madhubuti, nimeguswa kuongelea silaha za kujikinga na wachawi na majini.

Kila mtu anaweza kurogwa hasa asipojikinga kwa kinga hizi ninazokwenda kuzizungumzia.

Na ikiwa utampata mchawi hali ya kuwa anazifuata kinga hizi basi jua hiyo ni katika qadari zake Allah.

KINGA DHIDI YA SIHIRI

Yaeleweka kuwa Sihiri(Uchawi) na mafundo,  mara nyingi huwapata watu hasa wanapoishi katika jamii iliyo na wachawi waovu.

Hapa linakuja swali : “Je, yawezekana mtu kujikinga dhidi ya Sihiri hata akifanyiwa Sihiri hataweza kuathirika?”  Jawabu ndio. Hilo lawezekana na nitazitaja kinga hizi Insha-Allah

KINGA ZENYEWE NI HIZI :-

  • Kinga ya kwanza : Utakula tende saba za ‘ajwah (aina ya tende nzuri mno) kabla ya kula chakula. Ukiweza ziwe ni tende za madina itakuwa bora,  usipoweza basi tende yoyote ya ‘ajwah utakayoipata ni sawa.

Mtume(Rehma na amani za Allah ziwe juu yake) Amesema : “atakayekula asubuhi tende saba za ajwah, katika siku hiyo hatodhurika na sumu wala sihiri” . (Bukhari(10/249)

  • Kinga ya pili :  Kujilinda wakati wa kuingia chooni. Shetanai huwa akiotea fursa ya Muislamu kuwa chooni katika mahali pachafu ambapo ndipo maskani ya mashetani ya mashetani .
  • Kinga ya Tatu : Udhu.  Sihiri haimuathiri Muislamu aliyetawadha. Muislamu aliyetawadha amehifadhiwa na Malaika watokao kwa Allah.

‘Abdullah bin ‘Abbas amesimulia : Mtume (Rehema na amani za Allah ziwe juu yake) Amesema : “Vitwaharisheni viwiliwili hivi,  Allah atawatwahirisha. Hakuna mja anayelala ilihali yuko twahara ispokuwa Malaika hulala nayekatika nguo yake ya ndani. Hatogeuka wakati wowote usiku isipokuwa huomba : “Ewe Mola,  msamehe mja wako;  kwani alilala akiwa twahara(Tabarany,  isnadi yake ni jayyid kama alivyosema al-Mudhiry katika at-Targhib : 2/13)

  • Kinga ya Nne : Kuyafunga maisha ya unyumba kwa swala. ‘Abdullah bin Mas’ud amesema :Unapomwendea mkeo,  yaani siku ya kuingia kwake,  mwamuru aswali nyuma yako rakaa mbilii,  yaani umswalishe rakaa mbili,  Wewe uwe Imamu,  yeye maamuma na useme : “Allahumma baariklii fii ahlii wa baarik lahum fiyya. Allahummaj-ma” bainana ma jama “ta bikhairin, wa farriq bainana idha farraqta ilal-khairi.
  • Kinga ya Tano : Kumkinga mwanamke wakati wa kufunga naye ndoa. Baada ya kufunga ndoa na mkeo,  weka mkono wako wa kulia juu ya kipaji chake na useme ; “Allahumma inni as-aluka khairaha,  wakhaira ma jabaltaha alaih,  wa-auudhu bika min sharriha washarri ma jabaltaha alaih”, Mola wangu nakuomba kheri yake (mke) huyu na kheri ya maumbile ulivyomuumba nayo.  Najilinda kwako shari yake na shari ya maumbile uliyomuumba nayo.

Kwa wenye kuhitaji kusomewa visomo vya dua,  majinni na mashetani,  Muone Ostadh Nurdini : 0755 79 33 35

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s