SAIGON AMRUDIA ALLAH

saigon-before-and-after

Saigon kabla na baada ya kumrudia Mwenyezi Mungu

Rapa na mtangazaji mashuhuri nchini Tanzania, Saleh Daud Suleiman, maarufu kama SAIGON ameamua kumrudia Muumba wake na kuachana na mambo ya kidunia.

Akifahamika enzi hizo katikati ya miaka ya 2000, Saigon, alijizolea umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha ‘HipHop Base’ kilichokuwa kinaruka hewani kupitia kituo cha luninga cha East Africa ambacho kilitokea kupendwa zaidi na vijana.

Akizungumza na Redio Imaan kwenye kipindi cha inawezekana,  amesema kazi ya kumtumikia Mwenyezi Mungu ni kazi ngumu, huwezi kupigiwa makofi bali utapigwa mawe.

“Hii sio kazi ya kupigiwa makofi,  hii ni kazi ya kupigwa mawe na mti wenye matunda ndio wenye kupigwa mawe, kwaiyo ukiwa unafanya dawa  alafu watu wakakupigia makofi tu basi ujue dawa yako ina uwalakini”,  alisema Saigon.

Ameongeza kwamba amekuwa akitumiwa jumbe nyingi za simu kutoka kwa watu mbalimbali wakistaajabishwa na maisha yake mapya huku wengi wao wakimtakia heri na baraka za Mwenyezi Mungu azidi kumuongeza.

Mbali na Saigon wapo baadhi ya watu mashuhuri waliomrudia Allah, akiwemo Amir Junaid Hawkins A.K.A Loon aliyekuwa mwanamuziki wa lebo ya Bad boys chini ya mmiliki wake P.didy.

 

Advertisements

One response to “SAIGON AMRUDIA ALLAH

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s