IMAN ABDULATI – MWANAMKE MNENE ZAIDI DUNIANI

iman-abdulati

Iman Abdulati akiwa amelala kwenye kitanda chake.

Wahenga husema,”kuishi kwingi ni kuona mengi”, na kila siku zinavyozidi kwenda maajabu na vituko navyo havichezi mbali.

Katika pitapita zangu mtandaoni, nikabahatika kukutana na habari inayomuhusu mwanadamu  anayeshikilia rekodi ya kuwa mtu mnene  zaidi kuliko wote Duniani.

Anafahamika kwa jina la Iman Ahmad Abdulati,  mwanamke raia wa Misri mwenye umri wa miaka 36, akikadiriwa kuwa na uzito wa kilo zipatazo 500, akiwa amekaa zaidi ya miaka 25 pasipo kuliona jua, yaani bila kutoka nje.

Inatajwa kuwa alizaliwa na kilo 5, huku mwili wake ukisemekana kuhitaji kiasi kikubwa sana cha maji mwili zaidi ya uwezo wake.

Ndugu wa Iman walimwandikia barua Rais wa nchi hiyo, Abdel Fattah El-Sisi, wakimuomba awasaidie msaada wa matibabu.

Aidha barua hiyo ilionekana kuzaa matunda baada ya kufanikiwa kupata daktari nchini India aliyejitolea kumsaidia kumfanyia upasuaji(Gastic Surgery).

Kwa mujibu wa duru za habari nchini Misri, zimedai kwamba Iman alishindwa kupatiwa kibali cha kusafiri na ubalozi wa India kwa kile kilichoelezwa kuwa kushindwa kufika kwenye ofisi zao.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s